Milan mwenyeji wa Juventus ligi kuu Italia.


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 Italian Serie A

Matchday 9

AC Milan v Juventus FC

Stadio Giuseppe Meazza
Milano, Italy
Saturday, 8 October 2022
Kick-off is at 18h00  

AC Milan watakuwa mwenyeji wa Juventus FC katika mechi ya ligi kuu Italia Oktoba 8 ugani Stadio Giuseppe Meazza.

The Rossoneri kama wanavyofahamika Milan waliibuka na ushindi wa 3-1 ugenini dhidi ya Empoli FC katika mechi ya ligi iliyochezwa Oktoba 1.

Huu ulikuwa ushindi wa Milan wa pili ndani ya mechi tatu zilizopita huku wakipoteza mchezo mwingine dhidi ya SSC Napoli kabla ya kucheza na Empoli.

Ante Rebic
Hakimiliki ya picha: Getty Images


Matokeo dhidi ya Napoli yalifikisha kikomo msururu wa mechi 11 bila kushindwa kwa Milan kwenye mechi za ligi wakiwa nyumbani huku wakiandikisha sare tatu na kushinda mechi nane ugani Stadio Giuseppe Meazza.

Kwingineko, Juventus wakiwa nyumbani waliwaadhibu Bologna FC 3-0 kwenye mechi ya ligi iliyochezwa Oktoba 2.

Ushindi huo ulifikisha kikomo msururu wa mechi tatu za ligi bila ushindi kwa Juventus baada ya kuandikisha sare mbili na kushindwa mechi moja.

Juventus hawajapata ushindi kwenye mechi tano za mwisho za ligi ugenini baada ya kuandikisha sare mbili na kushindwa kwenye mechi tatu.

Massimiliano Allegri - Juventus manager
Hakimiliki ya picha: Getty Images


"Nimefurahia umoja tulioonyesha kwenye mchezo na kupata ushindi mkubwa na muhimu,” alisema meneja wa Massimiliano Allegri baada ya ushindi wa Bologna.

"Na pia kwa sababu hatukuwa tumepata ushindi kwa mwezi mmoja. Sharti tuwe makini kwa kuwa tulifanya maamuzi yasiyo sahihi kwenye mechi ya leo. Kuna nyakati tulitakiwa kupunguza kasi ya mchezo.

"Tutazidi kupambana kwa sababu hatupo kwenye nafasi nzuri Serie A na pia kwenye ligi ya UEFA.”

Mechi ya mwisho ya ligi baina ya Milan na Juventus ilikuwa Januari 23 2022. 

Mechi baina ya miamba hao wa soka wa Italia iliishia kwa sare ya 0-0 ugani Stadio Giuseppe Meazza.
 

Takwimu baina ya timu hizi mechi tano za mwisho za ligi

Mechi - 5
Milan - 2
Juventus - 1
Sare - 2
 

Ratiba ya mechi za Serie A mchezo wa tisa


Oktoba 8 Jumamosi

4:00pm - US Sassuolo v Inter Milan

7:00pm - AC Milan v Juventus FC

9:45pm - Bologna FC v UC Sampdoria

Oktoba 9 Jumapili

13:30pm - Torino FC v Empoli FC

4:00pm - AC Monza v Spezia Calcio

4:00pm - US Salernitana v Hellas Verona

4:00pm - Udinese Calcio v Atalanta BC

7:00pm - US Cremonese v SSC Napoli

9:45pm - AS Roma v US Lecce

Oktoba 10 Jumatatu

9:45pm - ACF Fiorentina v SS Lazio


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

 

Published: 10/07/2022