Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 Spanish La Liga
Matchday 11
Real Madrid v Sevilla FC
Estadio Santiago Bernabéu
Madrid, Spain
Saturday, 22 October 2022
Kick-off is at 22h00
Real Madrid atakuwa mwenyeji wa Sevilla FC katika
mechi ya ligi kuu Uhispania Oktoba 22 ugani Estadio Santiago Bernabéu.
The Whites walipata ushindi wa 3-1 nyumbani dhidi ya FC Barcelona kwenye mechi ya ligi iliyopita Oktoba 16 na watakuwa wageni wa Elche FC Oktoba 19.
Madrid hawajapoteza mechi yoyote ya ligi katika mechi 12 zilizopita huku wakiandikisha ushindi mara tisa na sare tatu.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Vile vile, Madrid hawajapoteza mechi yoyote ya ligi katika michezo minane iliyopita wakiwa nyumbani baada ya kuandikisha ushindi mara sita na sare mbili Estadio Santiago Bernabeu.
"Tumefurahishwa na ushindi huu pamoja na uchezaji wetu,” alisema kiungo wa Madrid Luka Modric baada ya ushindi dhidi ya Barcelona.
"Tulifahamu kuwa haitakuwa rahisi kwa sababu wanapenda kumiliki mpira. Ilitubidi kujituma zaidi na tulifanya hivyo.
"Juhudi zetu zilitupa magoli matatu. Tumefurahia uchezaji wetu. Kwa maoni yangu umeonyesha mchezo mzuri kabisa.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwingineko, Sevilla walipata ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Real Mallorca kwenye mechi yao ya mwisho ya ligi Oktoba 15 na walikuwa wenyeji wa Valencia CF Oktoba 18.
Ushindi dhidi ya Mallorca ulifikisha kikomo msururu wa mechi tatu bila ushindi kwa Sevilla baada ya kuandikisha sare mbili na kushindwa mara moja.
Hata hivyo, Sevilla hawajashindwa katika mechi tatu za ligi wakiwa ugenini huku wakiandikisha ushindi katika mechi mbili za kupata sare moja.
Mechi ya mwisho ya ligi kati ya Madrid na Sevilla ilikuwa Aprili 17 2022.
Madrid walipata ushindi wa 3-2 dhidi ya Sevilla ugani Estadio Ramon Sanchez-Pizjuan, uwanja uliotumika kuandaa nusu fainali ya kombe la dunia mwaka 1982.
Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi
Mechi - 5
Madrid - 4
Sevilla - 0
Sare - 1
Ratiba ya mechi La Liga mchezo wa 11
Oktoba 22 Jumamosi
3:00pm - Rayo Vallecano v Cadiz CF
5:15pm - Real Valladolid v Real Sociedad
7:30pm - Valencia CF v Real Mallorca
10:00pm - Real Madrid v Sevilla FC
Oktoba 23 Jumapili
3:00pm - RCD Espanyol v Elche CF
5:15pm - Real Betis v Atletico Madrid
7:30pm - Girona FC v CA Osasuna
7:30pm - Villarreal CF v UD Almeria
10:00pm - FC Barcelona v Athletic Bilbao
Oktoba 24 Jumatatu
10:00pm - Celta Vigo v Getafe CF
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.