Madrid na Barcelona kutoana kijasho El Clasico


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 Spanish La Liga

Matchday 9

Real Madrid v FC Barcelona 

Estadio Santiago Bernabéu
Madrid, Spain 
Sunday, 16 October 2022
Kick-off is at 17h15 

Real Madrid na Barcelona watafufua uhasama wao watakapokabiliana kwenye mechi ya ligi kuu Uhispania mnamo Oktoba 16 Estadio Santiago Bernabéu.
 
The Whites walipata ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya majirani wao katika mchezo wa ligi uliopita Oktoba 8.
 
Madrid hawajashindwa katika mechi 11 za ligi zilizopita huku wakiandikisha ushindi mara nane na kupata sare ya mechi tatu.

Carlo AncelottiHakimiliki ya picha: Getty Images

  
Vile vile, The Whites hawajashindwa katika mechi saba za ligi wakiwa nyumbani baada ya kuandikisha ushindi wa mechi tano na sare mbili Estadio Santiago Bernabeu.
 
"Kuna baadhi ya mechi zinazokuwa rahisi kucheza. Tulipata goli la mapema lililotupa utulivu kwenye mchezo huu,” alisema meneja wa Madrid Carlo Ancelotti baada ya ushindi dhidi ya Getafe.
 
"Tulidhibiti mechi vizuri kwa pasi nzuri na maamuzi mazuri japokuwa hatukufanikiwa kufunga magoli zaidi. Tumetengeneza nafasi nyingi za kufunga magoli kwenye mechi kadhaa zilizopita lakini hatujafunga magoli mengi.
 
“Mechi ya El Clasico bado ipo mbali. Kabla ya mechi hiyo kuna mechi nyingine. Ni nafasi ya kuwapa baadhi ya wachezaji fursa na kuwapumzisha waliocheza dakika nyingi.”

Raphinha
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kwingineko, Barcelona wakiwa nyumbani walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Celta Vigo kwenye mechi iliyopita ya ligi Oktoba 9.
 
Barcelona wameshinda mechi saba mfululizo na kupata sare moja kwenye mechi nane za ligi zilizopita.

vile vile, Barcelona hawajapoteza mechi yoyote ya ligi kati ya mechi 19 walizocheza ugenini huku wakiandikisha ushindi mara 14 na kupata sare tano.
 
Mchezo wa mwisho wa ligi baina ya Madrid na Barcelona ulichezwa Machi 20 2022.
 
Barcelona walipata ushindi wa 4-0 dhidi ya Madrid ugani Estadio Santiago Bernabéu ambao ulipewa jina hilo kwa heshima za mchezaji na rais wa zamani wa Real Madrid Santiago Bernabéu (1895–1978).
Takwimu baina ya timu hizi kwenye mechi 5 za mwisho za ligi.
Mechi - 5 
Madrid - 4
Barcelona - 1
Mechi - 0
 

Ratiba ya mechi za La Liga mchezo wa 9.  

 
Oktoba 14 Ijumaa
 
10:00pm - Rayo Vallecano v Getafe CF 
 
Oktoba 15 Jumamosi
 
3:00pm - Girona FC v Cadiz CF 
 
5:15pm - Valencia CF v Elche CF 
 
7:30pm - Real Mallorca v Sevilla FC
 
10:00pm - Athletic Bilbao v Real Madrid 
 
Oktoba 16 Jumapili
 
3:00pm - Celta Vigo v Real Sociedad
 
5:15pm - Real Madrid v FC Barcelona
 
7:30pm - RCD Espanyol v Real Valladolid 
 
10:00pm - Real Betis v UD Almeria 
 
Oktoba 17 Jumatatu
 
10:00pm - Villarreal CF v CA Osasuna
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.


Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 10/14/2022