Inter kukutana na Barcelona katika mechi ya kuvutia, UEFA


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 UEFA Champions League 

Group C

Inter Milan v FC Barcelona

Stadio Giuseppe Meazza 
Milan, Italy 
Tuesday, 4 October 2022 
Kick-Off is at 21h00  
 
Inter Milan na Barcelona watamenyana vikali katika mechi ya UEFA kundi C Oktoba 4.
 
Miamba hao wa Italia wakiwa ugenini walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Viktoria Plzen ya Jamhuri ya Czech katika mechi yao ya mwisho ya shindano hili Septemba 13.
 
Huu ulikuwa ni ushindi wa Inter Milan wa pili katika mechi tatu za mwisho za shindano hili, huku wakipoteza mchezo wa tatu dhidi ya mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich.

Hakan Çalhanoğlu
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Inter hawajapata ushindi wowote katika mechi mbili za mwisho wakiwa nyumbani katika shindano hili huku wakipoteza mechi zote mbili nyumbani mfululizo.
 
Kwingineko Barcelona walipoteza mechi yao ya mwisho ya UEFA wakiwa nyumbani 2-0 dhidi ya Bayern Munich Septemba 13.
 
Ilikuwa ni mechi ya pili kupoteza kwa miamba hao wa soka wa Uhispania katika mechi tatu za mwisho za shindano hili huku ushindi pekee ukija dhidi ya Viktoria Plzen.
 
Barca hawajapata ushindi wowote katika mechi mbili za mwisho za shindano hili wakiwa ugenini baada ya kupoteza mechi zote mbili.

XaviHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
“Tulicheza vizuri ukilinganisha na Bayern. Tulimiliki mpira vizuri katika kipindi cha kwanza. Hatuwezi kuwapa wapinzani wetu nafasi za kucheza kama tulivyofanya leo. Sina furaha kwa sababu ushindi ulikuwa wetu lakini tukazembea,” alisema meneja wa Barcelona Xavi Hernandez.

“Tulikuwa na mchezo mzuri ambao ungetupa ushindi. Tumejifunza japokuwa kwa makosa yetu. Hatukufunga goli hata baada ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga. Sina raha na motokeo ila nimefurahishwa na uchezaji wetu. Tulipambana nao vilivyo lakini mwisho wa siku matokeo yanahitajika.
 
"Walipata goli la kwanza kutokana na mkwaju wa kona na la pili lilitokana na uzembe wa kutokabili mashambulizi ya kushtukiza. Umakini unatakiwa kwa asilimia mia moja. Bayern ni timu nzuri ila sisi ndio mwanzo wa kutengeneza timu yetu. Kuna mambo tunayotakiwa kufanyia kazi na kuimarisha.”
 
Mchezo wa mwisho baina ya Barcelona na Inter katika shindano hili ulikuwa mnamo Disemba 10 2019.
 
Barcelona walipata ushindi wa 2-1 katika mechi hiyo ya kusisimua iliyochezewa ugani Stadio Giuseppe Meazza. 
 

Takwimu baina ya timu hizi kwenye mechi za UEFA.

Mechi - 10
Inter - 1
Barcelona - 6
Sare - 3
 

Ratiba ya mechi za UEFA mchezo wa tatu

 
Oktoba 4 Jumanne

7:45pm - Bayern Munich v Viktoria Plzen
7:45pm - Olympique Marseille v Sporting Lisbon
10:00pm - Liverpool FC v Rangers FC 
10:00pm - Ajax Amsterdam v SSC Napoli
10:00pm - Porto v Bayer Leverkusen
10:00pm - Club Brugge v Atletico Madrid
10:00pm - Inter Milan v FC Barcelona
10:00pm - Eintracht Frankfurt v Tottenham Hotspur

Oktoba 5 Jumatano

7:45pm - RB Salzburg v Dinamo Zagreb
7:45pm - RB Leipzig v Celtic FC 
10:00pm - Chelsea v AC Milan
10:00pm - Real Madrid v Shakhtar Donetsk
10:00pm - Manchester City v FC Copenhagen
10:00pm - Sevilla FC v Borussia Dortmund
10:00pm - Juventus v Maccabi Haifa
10:00pm - Benfica v Paris Saint Germain (PSG)


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 
 

Published: 10/03/2022