Foxes watafuta mbinu za kumzuia Haaland


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 14

Leicester City v Manchester City

King Power Stadium
Leicester, England
Saturday, 29 October 2022
Kick-off is at 14h30  

Manchester City watakuwa na nafasi ya kuongoza jedwali la ligi japo kwa muda watakaposafiri kuikabili Leicester Oktoba 29, Jumamosi.

The Citizens walipata ushindi wa 3-1 dhidi ya Brighton Jumamosi iliyopita baada ya kupoteza mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Liverpool, na sasa wapo nyuma ya viongozi wa ligi Arsenal kwa alama mbili. 

Erling Haaland alifunga magoli mawili na kuendeleza msururu wake wa ufungaji mabao ikiwa amefunga magoli 17 katika mechi 11 za ligi msimu huu.

Kevin De BruyneHakimiliki ya picha: Getty Images


Meneja wa City Pep Guardiola anahisi kuwa Haaland atavunja rekodi ya magoli mengi kufungwa ndani ya msimu wa ligi ya premier inayoshikiliwa kwa pamoja na Allan Shearer na Andy Cole, ambao walifunga magoli 34, 1994 na 1995 mtawalia.

"Hili lipo wazi kabisa. Akiendelea na kasi hiyo na wastani huo katika kila mechi atavunja rekodi,” alisema Guardiola.

"Anafurahi sana timu inaposhinda tofauti na tukipoteza mechi. Nimeshuhudia washambuliaji wengi kama Samuel Eto'o, David Villa, Lionel Messi, Robert Lewandowski, Thomas Muller na Sergio Aguero wenye uchu wa kufunga magoli mengi. Hilo ni jambo la kawaida.”

Shinikizo linaonekana kupungua kwa meneja wa Leicester Brendan Rodgers baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Wolves siku ya Jumapili, ambao ni ushindi wa tatu mfululizo katika ligi.

The Foxes walikuwa hawajapata ushindi katika mechi saba za kwanza msimu ila ushindi wa mechi tatu kati ya mechi tano zilizopita umewaweka Leicester katika nafasi ya 16, alama mbili juu ya mstari wa kushushwa daraja.

Jamie Vardy alipata goli lake la kwanza la msimu katika ushindi dhidi ya Wolves na kuwa mchezaji wa kwanza kufikisha magoli 100 moja baada ya kufikisha miaka 30.

Jamie VardyHakimiliki ya picha: Getty Images


Rodgers alisifia uchezaji mzuri wa timu yake baada ya kucheza mechi tatu mfululizo bila kuruhusu goli na kupata ushindi kwenye mechi iliyokuwa ngumu.

"Nimefurahi sana. Walicheza vizuri sana katika mechi iliyokuwa na changamoto,” alisema Rodgers. Tulionyesha uwezo wetu katika nyakati za magoli yote manne. Magoli yote yalitokana na maamuzi mazuri.

"Hii ni mechi ya nne ambayo hatujaruhusu goli katika mechi tano za mwisho za ligi tulizocheza. Ni wakati mwafaka wa kuwa na mwanzo mpya. Sharti tuzuie himaya yetu vizuri.

"Ni kikosi kizuri kilichokuwa na mwanzo mgumu wa ligi. Kwa sasa tunazuia vizuri na kuonyesha ukakamavu na kuonyesha uchezaji mzuri tunapokuwa tunamiliki mpira.”


Takwimu baina ya timu hizi kwenye mechi tano za mwisho za ligi

Mechi - 5
Leicester - 1
Man City - 4
Sare - 0
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 10/29/2022