Dortmund na matumaini ya kuzima makali ya City


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 UEFA Champions League

Group stage
Matchday 5

Borussia Dortmund v Manchester City

Signal Iduna Park
Dortmund, Germany
Tuesday, 25 October 2022
Kick-off is at 22h00  
 
Manchester City wanatarajia kuendeleza msururu wa matokeo mazuri ya mechi za UEFA msimu huu watakapoikabili Borussia Dortmund kwenye mechi ya makundi Oktoba 25 Jumanne Signal Iduna Park.
 
The Citizens walishinda mechi za kwanza tatu za kundi G kabla ya kulazimishwa sare ya 0-0 na FC Copenhagen, Copenhagen kwenye mchezo wa nne.
 
Alama waliyoipata iliwawezesha kuingia hatua ya muondoano japo vijana wa Pep wangependa kuchukua nafasi ya kwanza ya kundi hilo kabla ya kukutana na Sevilla katika mchezo wa sita.

Erling Haaland
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
City walilazimika kucheza na wechezaji 10 kwa dakika 60 ugani Parken Stadium baada ya Sergio Gomez kuonyeshwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza. Pep aliwasifia kwa ukakamavu walioonyesha licha ya kucheza na idadi ndogo ya wachezaji uwanjani.  
 
"Nimefurahi sana. Sio rahisi kucheza na wachezaji 10 dhidi ya 11 hasa kwenye mechi za UEFA,” Pep alisema baada ya sare hiyo.
 
"Tutapumzika na kujiandaa kwa ajili ya mechi zinazofuata. Tutakuwa ugenini dhidi ya Dortmund kusaka matokeo na kisha dhidi ya Sevilla tutakuwa tunatafuta matokeo ya kuongoza kundi.
 
"Baada ya matukio kama goli kukataliwa, penalti na kadi nyekundu mchezo ulibadilika na haikuwa rahisi kucheza wachezaji kumi dhidi ya kumi na moja kwa dakika 60.
 
"Wachezaji walijituma sana na kupata alama moja muhimu.”
 
Dortmund wapo katika nafasi ya pili, alama tatu nyuma ya City baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya Sevilla kwenye mchezo wa mwisho wa shindano hili.
 
Vijana wa Edin Terzic walipoteza 2-1 dhidi ya City katika mchezo wa pili ambapo Erling Haaland alipata bao dhidi ya waajiri wake wa zamani.  

Marco Reus
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Terzic alisistiza kuwa sare dhidi ya Sevilla yalikuwa matokeo mazuri ukizingatia ugumu wa mechi ila alionya kuwa hawawezi kucheza hivyo dhidi ya mabingwa wa England, City kwenye mwezo unaofuata.
 
"Timu zote hazikuonyesha mchezo mzuri. Hakuna nafasi nyingi za kufunga magoli zilizotengenezwa,” alisema mjerumani huyo baada ya mechi.
 
"Hatukufanya maamuzi mazuri kwenye pasi. Ilituchukua muda kufanya maamuzi uwanjani kwa hivyo katika hali hiyo sare ilitufaa. Tunahitaji kucheza vizuri na kufanya maamuzi sahihi wakati wa mechi.”
 

Takwimu baina ya timu hizi.

Mwchi - 5
Dortmund - 1
Man City - 3
Sare - 1
 

Ratiba ya mechi za UEFA Champions League mchezo wa 5.

 
Jumanne:
 
7:45pm: RB Salzburg v Chelsea
 
7:45pm: Sevilla v FC Copenhagen
 
10:00pm: Dinamo Zagreb v AC Milan
 
10:00pm: Celtic v Shakhtar Donetsk
 
10:00pm: RB Leipzig v Real Madrid
 
10:00pm: Borussia Dortmund v Manchester City
 
10:00pm: Paris Saint-Germain v Maccabi Haifa
 
10:00pm: Benfica v Juventus
 
Jumatano:
 
7:45pm: Club Brugge v FC Porto
 
7:45pm: Inter Milan v Viktoria Plzen
 
10:00pm: Napoli v Rangers
 
10:00pm: Ajax v Liverpool
 
10:00pm: Atletico Madrid v Bayer Leverkusen
 
10:00pm: Barcelona v Bayern Munich
 
10:00pm: Tottenham Hotspur v Sporting CP
 
10:00pm: Eintracht Frankfurt v Marseille
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

 
 
 

Published: 10/24/2022