Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 UEFA Champions League
Group stage
Matchday 4
Barcelona v Inter Milan
Camp Nou
Barcelona, Spain
Wednesday, 12 October 2022
Kick-off is at 20h00
Barcelona wana kibarua cha ziada katika azma yao ya kufuzu kuingia hatua ya muondoano ya
mechi za UEFA watakapomkaribisha Inter Milan Camp Nou Jumatano Oktoba 12.
The Blaugrana walipata kipigo cha 1-0 dhidi ya Inter Milan, maarufu kama Nerazzurri mjini Milan katika mchezo wa tatu wa shindano hili msimu huu. Hii ilikuwa mechi ya pili ya kundi C kwa Barcelona kupoteza mfululizo.
Vijana wa Barca chini ya Xavi wapo nyuma ya viongozi wa kundi hilo Bayern Munich na alama sita baada ya mechi tatu. Katika hali hiyo, ni sharti Barcelona kushinda mechi tatu zilizosalia ili kubaki kwenye shindano hili.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Xavi alionyesha wasiswasi wake katika nafasi iliopo timu yake kufuzu hatua inayofuata baada ya kuonyesha mchezo duni dhidi ya Inter na kukosa kufunga magoli kwenye mchezo uliopita.
"Matokeo ya mechi hiyo yananisikitisha. Hali sio rahisi,” alisema Xavi. “Wetu uliimarika dakika za mwisho na hatukuwa na mtiririko.
"Tulitengeneza nafasi lakini hutukuweza kuzitumia vizuri. Tulifahamu uwezo wao wa kupiga mashuti nje ya kisanduku. Tuna michezo mitatu iliyosalia ambayo itakuwa kama kucheza fainali. Kwa sasa nafasi yetu haifurahishi. Lazima tuongeze juhudi.”
Inter Milan wapo katika nafasi nzuri kufuzu hatua inayofuatayo baada ya kujizoa waliposhindwa kwenye mechi ya kwanza 2-0 na Bayern Munich na kushinda mechi mbili zilizofuata.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Inter chini Simone Inzaghi wapo alama tatu mbele ya Barca na kocha huyo amewasihi wachezaji wake kuonyesha ukakamavu kwenye michezo iwapo wana nia na mataji msimu huu.
"Tulitarajia hili,” Inzaghi aliambia kituo cha Sky cha Italia. “Jana nilisema kuwa hii ni fursa nyingine dhidi ya mojawapo ya timu bora duniani.
"Tulicheza kwa kasi na dhamira kwani ndio njia pekee ya kushinda dhidi ya timu sampli hii. Tumesubiri nafasi hii kwa muda. Nina furaha tumeleta tabasamu kwa mashabiki na klabu kwa ujumla lakini safari bado.
"Ni matumaini yangu jioni ya leo itaashiria mwanzo wa mafanikio zaidi. Hilo linawezekana ila tunahitaji kuonyesha juhudi zaidi na ukakamavu kama tulivyofanya leo.”
Takwimu baina ya timu hizi:
Mechi - 15
Barcelona - 8
Inter Milan - 3
Sare - 4
Ratiba ya mechi za UEFA mchezo wa 4
Jumanne:
7:45pm: FC Copenhagen v Manchester City
7:45pm: Maccabi Haifa v Juventus
10:00pm: Dinamo Zagreb v RB Salzburg
10:00pm: AC Milan v Chelsea
10:00pm: Shakhtar Donetsk v Real Madrid
10:00pm: Celtic v RB Leipzig
10:00pm: Borussia Dortmund v Sevilla
10:00pm: Paris Saint-Germain v Benfica
Jumatano:
7:45pm: Napoli v Ajax
7:45pm: Atletico Madrid v Club Brugge
10:00pm: Rangers v Liverpool
10:00pm: Bayer Leverkusen v Porto
10:00pm: Barcelona v Inter Milan
10:00pm: Viktoria Plzen v Bayern Munich
10:00pm: Tottenham v Eintracht Frankfurt
10:00pm: Sporting CP v Marseille
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.