Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Italian Serie A
Matchday 11
Hellas Verona v Juventus FC
Stadio Marc'Antonio Bentegodi
Verona, Italy
Saturday, 30 October 2021
Kick-off is at 19h00
Oktoba 30 Hellas Verona itawaalika Juventus uga wa nyumbani Stadio Marc’Antonio Bentegodi katika mchezo wa ligi kuu ya
Serie A, Italia.
Verona ilitoka sare ya 1-1 ikiwa ugenini dhidi ya Udinese Calcio katika mchezo wa ligi uliochezwa Oktoba 27.
Kwa sasa Verona wameepuka kushindwa katika mechi mbili za ligi zilizopita huku wakiambulia sare moja na kushinda mechi moja.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Vile vile, Verona wameshinda mechi tatu za ligi mfululizo wakiwa nyumbani.
Kwingineko, wakiwa nyumbani, Juventus walipoteza mchezo wao wa ligi 2-1 dhidi ya UD Sassuolo kwenye mechi iliyochezwa tarehe 27 Oktoba.
Matoke ohayo yanamaanisha bibi kizee hajapata ushindi katika mechi mbili za ligi zilizopita baada ya kutoka sare na kupoteza mechi moja.
Hata hivyo, Juventus hawajapoteza mchezo wowote ugenini kati ya mechi tatu walizocheza huku wakipata sare moja na kushinda mechi mbili mfululizo.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Tatahitaji kufunga magoli mengi kwa sababu goli moja katika mechi halitoshi,” alisema Massimiliano Allegri wa Juventus baada ya kupoteza mechi dhidi ya Sassuolo.
“Tunahitaji kujiweka sawa na kuwa na mchezo endelevu wakati wa kushambulia na kuzuia wakati wote. Hatuwezi kuendelea kupoteza mechi jinsi tunavyofanya sasa. Inatubidi tuweke mikakati kupata suluhu ya matatizo yetu.
“Ukweli ni kwamba inatupasa kucheza vizuri zaidi kuliko tunavyocheza kwa sasa. Tunahitaji kuwa pamoja zaidi sasa hivi kama kikundi. Ni muhimu tuweke pembeni matokeo haya haraka iwezekanavyo kwa sababu tunao mchezo mwingine mgumu jumamosi.”
Mechi ya ligi ya mwisho baina ya timu hizi mbili ilikuwa Februari 27 2021.
Katika mechi hiyo iliyochezewa ugani Stadio Marc’Antonio Bentegodi, timu hizo ziliambulia sare ya 1-1
Takwimu baina ya timu hizi katika mechi tano za ligi za mwisho
Mechi - 5
Verona - 1
Juventus - 2
Sare - 2
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway