The Foxes na Red Devils wapania matokeo bora


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Ligi kuu ya England 

Matchday 8 of 38

Leicester City vs Manchester United 

King Power Stadium 
Leicester, England
Saturday, 16 October 2021
Inaanza 17:00 
 
Baada ya kukosa ushindi kwenye mechi kadhaa zilizopita za ligi kuu Uingereza msimu huu, Leicester City na Manchester United wanapania kupata ushindi kila mmoja watakapo kutana katika uwanja wa King Power stadium jumamosi hii.

Ole Gunnar Solskjaer
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
‘The Foxes’, kama wanavyofahamika Leicester City hawajapata ushindi katika mechi nne za ligi huku wakiruhusu mabao mawili dakika za mwisho mwisho na kutoka sare walipocheza na Crystal Palace katika mechi ya mwisho kabla ya ligi kuchukua mapumziko madogo.
 
Matokeo haya yamewaacha katika nafasi ya kumi na tatu katika jedwali la ligi mbali kabisa na matarajio yao msimu utakapokamilika.
 
Kwa upande wao, united hawajapata ushindi kwenye mechi mbili zilizopita. Baada ya kupoteza nyumbani dhidi ya Aston Villa na kulazimisha sare dhidi ya Everton ugani Old Trafford, kwa sasa The Red Devils wako pointi mbili nyuma ya vigogo wa ligi Chelsea. 
 
‘Nadhani tulicheza vizuri sana kipindi cha kwanza na kuwa na nafasi nyingi za kufunga mabao lakini kipindi cha pili tukatetereka. Kwa mara nyingine tukarudia yale makosa’,. Haya ni maneno ya kiungo wa United Bruno Farnandes akizungumza na MUTV baada ya kutoka sare Everton, kwa jina la utani the Toffees
 
“Ni lazima tujifunze kutokufanya makosa kama haya na wakati ni sasa. Tumerudia makosa haya safari nyingi sana. Hatuwezi kupunguza kasi na hari ya mchezo tunapowazidi wapinzani wetu. Inabidi tuongeze kasi sana na tufunge mabao Zaidi kisha tunaweza kutuliza kasi ya mechi na kuwachosha Zaidi.
 
“Hatujacheza vizuri sana na tunapaswa kuwa na pointi Zaidi ya tulivyo sasa. Ni lazima tujitume sana kisha tutakuwa wapi ifikiapo mwisho wa msimu,”. Aliongeza

Bruno Fernandes
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Leicester city walichukua pointi nne kutoka kwa Manchester united msimu uliopita huku wakipata sare ya 2-2 nyumbani kabla ya kuwashinda United 2-1 ugani Old Trafford.
 

Takwimu za matokeo baina ya timu hizi mbili

 
Mechi – 96
 
Leicester – 24
 
Manchester United - 48
 
Sare - 24
 

Mechi zitakazochezwa wikendi hii, mchezo wa siku ya 8

 
Oktoba 16 Jumamosi
 
14:30 - Watford vs Liverpool
17:00 - Southampton vs Leeds United
17:00 - Norwich City vs Brighton & Hove Albion
17:00 - Aston Villa vs Wolverhampton Wanderers 
17:00 - Leicester City vs Manchester United
17:00 - Manchester City vs Burnley
19:30 - Brentford vs Chelsea
 
Oktoba 17 Jumapili
 
16:00 - Everton vs West Ham United
18:30 - Newcastle United vs Tottenham Hotspur
 
Oktoba 18 Jumatatu
 
22:00 - Arsenal vs Crystal Palace

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway
 

Published: 10/13/2021