Red Devils kuja na makali baada ya kutandikwa na Liverpool nyumbani


Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 

2021/22 English Premier League

Matchday 10 of 38

Tottenham Hotspur vs Manchester United 

Tottenham Hotspur Stadium 
London, England
Saturday, 30 October 2021 
Kick-off is at 19:30 

Manchester united wanapania kupata matokeo mazuri watakapokutana na Tottenham Hotspurs Jumamosi hii baada ya kupata kichapo kikali mikononi mwa Liverpool kwenye mchezo wa ligi kuu Engalnd msimu huu wa 2021/22.


Luke Shaw
Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 
 
Mashetani wekundu walipoteza mchezo wao wa ligi dhidi ya mahasidi wao wa jadi Liverpool kwa magoli 5-0 Jumapili iliyopita matokeo ambayo yanaipeleka klabu hiyo ya Manchester kutokuwa na ushindi katika mechi nne za ligi. Kwa sasa wanachukua nafasi ya saba katika msimamo wa ligi wakiwa alama nane nyuma ya vigogo Chelsea ambao ndio viongozi huku shinikizo likizidi kwa meneja Ole Gunnar Solskjear.
 
“Tunaweza kusema kwamba tulitarajia matokeo haya,” alisema mlinzi wa kushoto wa United Luke Shaw baada ya kipigo kutoka kwa Liverpool. “Hata mechi tulizoshinda awali hatujaonyesha mchezo mzuri na wote tunalifahamu hilo.
 
 
“Tunahitaji kuchambua nini kiini na kuendelea mbele kwani matokeo haya yanaumiza. Ni mambo ambayo tuliteta katika chumba ya kubadilishia.”
 
 
Kwa maoni ya Shaw, lawama ya matokeo yao mabaya isielekezwe tu kwa mkufunzi bali pia wachezaji na mapungufu yao wanachangia.
 

“Kwa maoni yangu, tunahitaji kujitathmini sisi wenyewe,” aliongeza. Je, tunajiandaa vizuri na kufanya kila kitu ipasavyo ili kuikabili timu pinzani?
 
 
“Tunazo mbinu na njia ya kucheza kama atakavyo mkufunzi wetu lakini nahisi kwamba wakati mwingine tunapoteza muelekeo na tunawafanyia wepesi wapinzani wetu.”
 
Spurs wamepoteza michezo minne ya ligi kati ya sita iliyopita huku mchezo wao wa wikendi iliyopita wakipigwa na West Ham United.

Harry Kane
Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 
 
Msimu uliopita Manchester united walipoteza mchezo wao na Tottenham kwa magoli 6-1 nyumbani kisha wakapata ushindi wa magoli 3-1 ugenini katika mechi ya marudiano.
 

Takwimu baina ya timu hizi mbili katika michezo ya ligi

 
Mechi: 166
Tottenham Hotspur: 39
Manchester United: 87
Sare: 40
 

Ratiba ya mechi za ligi kuu Engalnd, mchezo wa siku ya 10

 
Jumamosi, 30 Oktoba 
 
14:30 - Leicester City vs Arsenal 
17:00 - Watford vs Southampton
17:00 - Liverpool vs Brighton & Hove Albion 
17:00 - Newcastle United vs Chelsea 
17:00 - Manchester City vs Crystal Palace 
17:00 - Burnley vs Brentford 
19:30 - Tottenham Hotspur vs Manchester United 
 
Jumapili, 31 Oktoba
 
17:00 - Norwich City vs Leeds United
19:30 - Aston Villa vs West Ham United 
 
Jumatatu, 01 Novemba
 
22:00 - Wolverhampton Wanderers vs Everton 

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 10/28/2021