Milan kuwakaribisha vijana wanaojituma sana wa Verona


Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 

2021/22 Italian Serie A

Matchday 8

AC Milan v Hellas Verona 

Stadio Giuseppe Meazza 
Milano, Italy 
Saturday, 16 October 2021
Kick-off is at 21h45 


AC Milan watamenyana na Hellas Verona oktoba kumi na sita  katika mechi ya ligi ya Italia, Serie A ugani Stadio Giuseppe Meazza
 
Maarufu kama “The Reds and Blacks”, Milan walipata ushindi wa magoli matatu kwa mawili dhidi ya Atalanta katika mchezo uliopita wa ligi wa tarehe tatu oktoba.
 
Baada ya ushindi huu, Milan imecheza mechi kumi na mbili za ligi bila  kupotela. Wameshinda mara kumi na kutoka sare mara mbili

Stefano Pioli
Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 
 
Vile vile, Milan hawajapoteza mchezo wowote wa ligi nyumbani kati ya mitano ya mwisho huku wakiambulia ushindi mara nne na kutoka sare mara moja.
 
“Nimeimarika pia. Hii inachangiwa na kuwa na kikosi kizuri, mashabiki na wakurugenzi wanaoniunga mkono. Haya ni maneno ya Stefano Pioli baada ya ushindi wa Milan dhidi ya Atalanta 
 
“Tunapofanya kazi wote kwa pamoja mambo yanakuwa rahisi. Lakini hii ni safari ndefu na tunahitaji kujituma na kunyenyekea kwa sababu hivi ni vita.
 
“Wakati huo huo, ni vizuri kwenda na wimbi la umoja huu. Nataka wachezaji wangu kujihisi ni mahiri kuliko wengine. Sasa ni jukumu lao kudhihirisha hilo mechi baada baada ya mechi”

Matteo Lovato
Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 
 
Verona waliwakung’uta Spezia mabao manne bila jawabu nyumbani katika mechi ya ligi iliyochezwa oktoba tarehe tatu.
 
Verona, wanaojulikana kwa jina la utani kama “The Yellow and Blues” wameshinda michezo miwili na kwenda sare mara mbili kwenye michezo minne iliyopita ya ligi.
 
Licha ya mafanikio hayo, Verona hawajapata ushindi wowote katika michezo saba ya mwisho ya ugenini huku wakipoteza mara nne na kupata sare tatu.
 
Walipokutana kwa mara ya mwisho, Milani walipata ushindi wa mabao mawili katika mchezo wa ligi mnamo tarehe saba machi mwaka huu. Mechi iliandaliwa ugani Stadio Marc’Antonio Bentegodi.
 

Matokeo ya mechi tano za mwisho za ligi baina ya timu hizi mbilli

 
Mechi – 5
Milan – 3
Verona – 0
Sare – 2

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway
 

Published: 10/12/2021