Madrid wapania ushindi kwa timu ya Osasuna isiyotabirika


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Spanish La Liga

Matchday 10

Real Madrid v CA Osasuna 

Estadio Santiago BernabĂ©u
Madrid, Spain 
Wednesday, 27 October 2021
Kick-off is at 22h30  
 
Real Madrid itamenyana na CA Osasuna  Oktoba 27 ugani Estadio Santiago Bernabeu katika mechi ya ligi kuu nchini Uhispania.
 
 
Miamba hao wa Madrid waliinyuka FC Barcelona 2-1 ugenini katika mchezo wa ligi wa tarehe 24 Oktoba
 
 
Matokeo haya yalitia kikomo matokeo mabaya ya Madrid ya mechi mbili kabla, ambapo walikuwa wamepoteza mechi moja na kwenda sare mechi moja.

Carlo Ancelotti
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Madrid wamecheza mechi 13 nyumbani bila kupoteza mchezo wowote katika mechi za ligi huku wakipata ushindi mara 9 na kuambulia sare 4.
 
 
“Ulikuwa ni mchezo mgumu hivyo nimefurahisha na hizi alama tatu. Barcelona walitukabili vilivyo na ushindi wetu haukuja kirahisi,” alisema meneja wa Madrid Carlo Ancelotti baada ya kuiongoza timu yake kwenye ushindi huo dhidi ya Barcelona.
 
 
“Tunao uwezo wa kushindana. Timu yetu ni nzuri sana na lengo letu ni kuendelea kuboreka kila uchao na hiyo ndiyo mipango yetu. Ni muhimu pia kukumbuka kwamba tumecheza na timu nzuri ambayo imecheza mchezo mzuri.
 
 
“Ilibidi tujitume zaidi na tulifanya hivyo kwa pamoja. Tulipambana kuudhibiti mchezo nyakati zote; tulipomiliki mpira na walipoumiliki wao na hilo ni jambo la msingi.

Oier
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Kwa upande mwingine, katika mechi iliyochezwa Oktoba 22, Osasuna walitoka sare ya 1-1 na Granada nyumba ikiwa ni mchezo wao wa hivi karibuni.
 
 
Osasuna wamecheza mechi nne za ligi bila kupoteza mechi yoyote huku wakishinda mechi tatu mfululizo na kutoka sare mechi moja.
 
 
Ugenini, Osasuna hawajapoteza mechi yoyote ya ligi kati ya nne walizocheza huku wakishinda zote nne mfululizo.
 
Timu hizi kukutana mara ya mwisho katika ligi ilikuwa Mei 1 2021
 
Madrid walishinda mechi hiyo mabao 2-0 katika mechi iliyochezewa Estadio Alfredo Di Stefano ambayo ni sehemu mojawapo ya kufanyia mazoezi ya klabu ya Real Madrid.
 

Takwimu baina ya timu hizi mbili kwenye mechi tano za mwisho za ligi walizokutana

Mechi - 5 
Madrid - 4
Osasuna - 1
Sare - 0


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 10/26/2021