Madrid kuikabili timu ya Bilbao inayoimarika kila uchao


Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 

2021/22 Spanish La Liga

Matchday 9

Real Madrid v Athletic Bilbao 

Estadio Santiago BernabĂ©u
Madrid, Spain 
 
Klabu ya Real Madrid itachuana na Athletic Bilbao katika uwanja wa Estadio Santiago Bernabeu mnamo tarehe kumi na saba mwezi oktoba katika mechi ya ligi, La liga.
 
Katika hali ya kushangaza, Madrid walipoteza mchezo wao wa ligi waliponyukwa mabao mawili kwa moja ugenini dhidi ya Espanyol mchezo uliochezwa oktoba tarehe tatu.
 
Hawajapata ushindi kwenye mechi mbili zilizopita huku wakiambulia sare moja ikifuatiwa na ushinde dhidi ya Espanyol

Nacho
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Licha ya hayo, Madrid hawajapoteza mchezo hata mmoja wa ligi kati ya mechi kumi na tatu walizocheza nyumbani. Wamepata ushindi mara tisa na sare tisa nyumbani.
 
“Timu yetu ina majeruhi wengi lakini hii sio sababu kwa sababu tunacho kikosi kizuri cha kupata matokeo mazuri kuliko ya mechi hizi tatu zilizopita.” Alisema Nacho, mlinzi wa Real Madrid baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Espanyol.
 
“Timu inaposhindwa kuzuia magoli mchezo unakuwa mgumu Zaidi. Hakuna mechi rahisi katika ligi kuu ya Primera. Espanyol walijiandaa vizuri hivyo basi mambo hayakutuendea kama tulivyopanga sisi leo.
 
Hii wiki haikuwa nzuri ukizingatia matokeo. Tunaelekea kwenye mapumziko na tutatadhmini ili kubaini ni wapi tunafaa kurekebisha. Huu ni mwannzo wa ligi tu na tunahitaji kila mmoja wetu ajitume ili tupate matokeo mazuri.”
 
Wakati huo huo, Bilbao walipata ushindi wa goli moja bila jibu nyumbani katika mechi yao na Alaves. Hii ni katika mechi ya hivi maajuzi iliyochezwa tarehe moja oktoba.
 
Bilbao, maarufu kama “the lions” kwa jina la utani, hawajapoteza mchezo wowote kati ya miwili iliyopita ya ligi huku wakipata sare moja na ushindi mmoja.
 
Katika michezo minne ya ugenini iliyopita, Bilbao wamepata sare tatu ta kushinda mechi moja.
 
Walipokutana mara ya mwisho kwenye mechi ya ligi, Madrid walipata ushindi mwembamba wa bao moja dhidi ya Bilbao katika mechi iliyochezewa uga wa nyumbani wa Bilbao, Estadio San Mames.
 

Haya ni matokeo ya mechi tano za mwisho za ligi baina ya timu hizi mbili

Mechi – 5
Madrid – 4
Bilbao – 0
Sare – 1

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway
 

Published: 10/12/2021