Inter na Juventus kwenye debi ya Derby d'Italia


Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 

2021/22 Italian Serie A

Matchday 10

Inter Milan v Juventus FC 

Stadio Giuseppe Meazza 
Milano, Italy 
Sunday, 24 October 2021
Kick-off is at 21h45 
 
Oktoba 24 kutakuwa na mechi ya kukata na shoka, Inter Milan watakapo menyana na Juventus katika mechi ya ligi ugani  Stadio Giuseppe Meazza
 
The Big Grass Snake, kama wanavyojulikana Inter Milan walipoteza mchezo wao dhidi ya Lazio katika mchezo wa ligi uliopita kwa mabao 3-1 oktoba 16
 
Kushindwa kwa Inter milan kulifikisha kikomo mechi nane bila kushindwa huku wakiandikisha ushindi mara 6 na sare 2

Simone Inzaghi
Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 
 
Hata hivyo, Inter Milan hawajapoteza mchezo nyumbani kati ya michezo 20 ya ligi waliyocheza wakiwa na sare 2 na ushindi mara 18 mfululizo
 
 “Ulikuwa ni mchezo mzuri kwetu ukilinganisha na michezo mingine ya hivi karibuni lakini tunapokuwa tumefunga goli moja, tunatakiwa kuudhibiti mchezo vizuri na kuongeza mabao” alisema mkufunzi wa Inter Simone Inzaghi baada ya kushindwa na Lazio.
 
 “Ulikuwa ni mchezo wa kusisimua ulioisha kwa matokeo ambayo hatukufurahia kwa sababu tulithibiti mechi hiyo kwa nyakati tofauti na tungefunga magoli zaidi nap engine kuwa na magoli 2-0.”
 
 “kuna siku mbili za kuchambua mchezo huo kwa sababu hatufai kupoteza mchezo 3-1 baada ya kuonyesha mchezo mzuri kama tulivyoonyesha.

Moise Kean
Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 
 
Kwengineko Juventus walipata ushindi finyu wa goli 1-0 dhidi ya AS Roma katika mchezo wa ligi wa oktoba 17.
 
Juventus, maarufu kama Old Lady hajapoteza mchezo wa ligi kati ya mitano iliyopita baada ya kushinda mara nne mfululizo na kupata sare moja.
 
Ugenini, Juventus wamepata ushindi mara mbili katika mechi mbili za mwisho walizocheza.
 
Mei 15 2021 ndio mara ya mwisho ya timu hizi mbili kukutana
 
Mechi hiyo ilichezewa Juventus stadium ambao ndio uwanja wa sita kwa ukubwa Italia ambako Juventus waliibuka washindi kwa magoli matatu dhidi ya mawili ya Inter.
 

Takwimu baina ya timu hizi mbili katika mechi tano za ligi zilizopita.

Mechi - 5
Inter  - 1
Juventus - 3
Sare - 1


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway
 

Published: 10/19/2021