Elche wanuia kuzima ndoto ya ubingwa wa ligi wa Real Madrid


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Spanish La Liga

Matchday 12

Elche CF v Real Madrid 

Estadio Manuel Martínez Valero 
Elche, Spain
Saturday, 30 October 2021
Kick-off is at 15h00 
 
 
Elche CF na Real Madrid watakabana koo kwenye mchuano wa ligi utakaogaragazwa katika uwanja wa nyumbani wa Elche, Estadio Manuel Martinez Valero Oktoba 30.
 
 
Katika mechi ya ligi iliyochezwa Oktoba 26, Elche wakiwa ugenini walichapwa na Deportivo Alaves bao 1-0.
 
 
Hadi kufikia mechi iliyopita la ligi, Elche hawajapata ushindi wowote katika mechi tatu za mwisho walizocheza huku wakiambulia sare moja na kupoteza mechi mbili.
 

Gonzalo Verdu
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Matokeo ya Elche wakiwa nyumbani yamekuwa mazuri katika mechi sita za ligi zilizopita kwani wameweza kupata ushindi mara nne na kutoka sare mbili.
 
 
Kwingineko, Madrid walilazimishwa sare ya suluhu bin suluhu wakiwa nyumbani na timu ya CA Osasuna katika mechi iliyochezwa Oktoba 27.
 
 
Tukizingatia matokeo haya, Madrid haijapoteza mechi mbili za ligi zilizopita wakiandikisha ushindi wa mechi moja na kutoa sare moja.
 
 
 
Baada ya kwenda mechi 18 bila kushindwa ugenini, Madrid walipoteza mechi yao dhidi ya Espanyol lakini wakarudi tena kwa ukali na kuwalaza Barcelona Camp Nou.
 

Carlo Ancelotti
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
“Kipindi cha kwanza hatukuwa na mchezo mzuri kwani tulitumia kupita kiasi upande wa kushoto. Sikupenda,” haya ni maoni ya Carlo Ancelotti meneja wa Madrid baada ya sare na Osasuna.
 
 
“Tulijituma sana kipindi cha pili. Siwezi kuwalaumi wachezaji wangu kwa sababu walipambana iwezekanavyo. Tutakuwa na mechi ngumu kama hii katika ratiba yetu. Tunao wachezaji wenye uwezo binafsi  wa kuisaidia timu lakini wakati mwingine wapinzani wetu wanakuwa na mbinu dhabiti za kuwazuia. Ni lazima tutafakari kuhusu suluhisho ya mapungufu haya kwani tulijaribu mbinu nyingi lakini hatukufua dafu.”
 
 
Elche na Madrid walikutana kwa mara ya mwisho kwenye mechi ya ligi mwaka huu wa 2021 Machi 13
 
 
Elche walipoteza mchezo huo ambao ulichezewa katika uwanja wa Estadio Alfredo Di Stefano kwa magoli mawili huku wao wakifunga moja.
 

Matokeo ya mechi tano za mwisho baina ya timu hizi

 
Mechi - 5
Elche - 0
Madrid - 4
Sare - 1

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 10/29/2021