Bucks wafukuzia ushindi mechi ya kwanza ugenini


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

Miami Heat v Milwaukee Bucks

2021-22 NBA Regular Season

Friday 22 October 2021
FTX Arena, Miami, Florida
Tip-off at 03:00 
 
The Milwaukee Bucks watapania kupata ushindi katika mechi yao ya kwanza ya NBA msimu 2021/22 watakapochuana na Miami Heat ugenini ugani FTX Arena Miami Florida Ijumaa oktoba 22 2021 kuanzia saa nane asuhui majira ya Afrika ya kati

Katika kumalizia maandalizi ya msimu unaoanza, The Heat walishinda mchezo wa kirafiki dhidi ya Boston Celtics kwa alama 121-100 nyumbani wikendi iliyopita huku Jimmy Butler na Tyler Herro wakiizolea timu hiyo alama 25 na 29 mtawalia.
 
Hivi maajuzi, Herro amepokea ukosoaji kwa kudai kuwa NBA inastahili kumtambua katika kiwango kimoja na wachezaji mahiri  na chipukizi katika NBA kwa sasa lakini anatarajia kuonyesha mchezo mzuri utakaotetea kauli yake.

Giannis Antetokounmpo
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
 “Najihisi niko katika kiwango kimoja na hao vijana chipukizi katika ligi hii ambao watakuja kuwa nyota wakubwa siku za usoni – Luka(Doncic), Trae Ja(Young) na wengineo. Jina langu linastahili kuwa katika hii orodha pia,” alisema Herro. Najitahidi sana kila siku ili kuboresha mchezo wangu. Nina ndoto nyingi akilini mwangu; kuwa mchezaji mkubwa siku za usoni na kufukuzia malengo yangu. Ninayo furaha kubwa kuona uwezo wangu na mambo ambayo ninaweza kufanikisha.
 
Mabingwa wa NBA Milwaukee hawajakuwa na maandalizi mazuri ya msimu huku wakipoteza mechi za kirafiki dhidi Memphis Grizzlies, Brooklyn Nets na Dallas Mavericks lakini wanamatumaini kwamba watarudi kwenye mwendo wa ushindi msimu utakapoanza.
 
Jimmy Butler
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
 “Malengo ni yale yale,” alisema mkufunzi wa bucks Mike Budenholzer ambaye maajuzi aliongeza kantarasi yake kwa miaka mitatu hadi msimu wa 2024/25. 
 
“Tunafurahi matunda yetu tuliyopata kwa miaka mitatu. Tulishinda taji mwaka uliopita lakini wachezaji wetu wana uchu wa kuboreka kila siku.”
 
Takwimu zinaonyesha kwamba timu hizi mbili zimekutana mara 118 kwenye mechi za msimu wa kawaida kuanzia 1988/89. Miami wameshinda mara 71 ukilinganisha na mara 47 kwa faida ya Milwaukee. Kwenye mechi ya ligi ya mwisho, timu hizi zilikutana Mei 2021 ambapo Bucks walishinda 122-108.
 

Takwimu baina ya timu hizi mbili kwenye msimu wa kawaida

Mechi: 118
Heat: 71
Bucks: 47
 

Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.




Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 10/21/2021