Hakimiliki ya picha: Getty Images
Portland Trail Blazers v LA Clippers
2021-22 NBA Regular Season
Saturday 30 October 2021
Moda Center, Portland, Oregon
Tip-off at 05:00
Kutakuwa na kivumbi kikali cha
mpira wa kikapu Jumamosi hii Moda Center Portland Oregon wakati Portland Trail Blazers wataialika Los Angeles Clippers katika mechi ya msimu wa kawaida majira ya saa kumi asubui Oktoba 30 2021.
Mechi hii inakuja wakati tetesi kuhusu uhusiano baina ya mchezaji nyota Damian Lillard na Klabu yake ya Trail Blazers ikizidi kuzua gumzo lakini mchezaji huyo ameeleza hisia zake na kusema kwamba atasalia na klabu. “Watu wengi wamekuwa na maoni kuhusu Maisha yangu na klabu hii lakini niwahakikishie kwamba nitaendelea kuitumikia Portland,” alisema Lillard.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Akiongeza, Lillard alisema “Uamuzi wangu wa kuendelea kuitumikia timu hii umechangiwa sana na mazungumzo yangu na kocha Chauncey Billups ambaye wote tuna mwelekeo mmoja. Siwezi kusema tulizungumzia nini ila niliona kitu tofauti kwake katika mazungumzo yetu jambo ambalo halitokei mara nyingi kwangu.”
Clippers wamekosa huduma za mchezaji kisiki Kawhi Leonard kutoka mwanzo wa msimu huu wa 2021/22 kutokana na jeraha la goti na ambalo anaendelea kuliuguza.
Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amekuwa akiudhuria mikutano ya kiufundi na wachezaji wengine pamoja na kuwapa motisha uwanjani wanapocheza.
Photo suggestion: Portland Trail Blazers centre Cody Zeller
“ Nafikiri anataka kuwa mwalimu,” alisema kwa mzaha kocha wa Clippers Tyronn Lue. Amekuwa na ushawishi mkubwa katika timu yetu. Anatupa hari sisi sote na kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu anajikaza kuelekea upande mmoja. Anatumia muda na wakufunzi na kujifunza mambo mengi kuhusu ukufunzi. Ni faraja sana kuwa na yeye baina yetu.”
Trail Blazers na Clippers wamekutana mara 231 katika mechi za msimu wa kawaida kuanzia msimu wa 1970/71. Portlans wameshinda mara 147 huku Clippers wakishinda mara 84. Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa ni Aprili 2021 ambapo Clippers walishinda kwa alama 113 dhidi ya 112 za Blazers. Ushindi huu ulikuwa wa sita mfululizo dhidi ya Blazers ugenini.
Takwimu baina ya timu hizi mbili katika msimu wa kawaida
Mechi walizocheza: 231
Trail Blazers: 147
Clippers: 84
Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu,
mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.