Barcelona na Madrid kukutana kwenye debi ya El Clasico


Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 

2021/22 Spanish La Liga

Matchday 10

FC Barcelona v Real Madrid

Camp Nou
Barcelona, Spain 
Sunday, 24 October 2021
Kick-off is at 17h15
 
FC Barcelona watafufua uhasama wao na Real Madrid watakapo kutana kwenye mechi ya ligi ugani Camp Nou Oktoba 24.
 
Wakiwa nyumbani, Barcelona walitoka nyumba na kuishinda Valencia mabao 3-1 kwenye mchezo wa ligi uliopita wa tarehe 17 oktoba.
 
Kabla ya ushindi huo dhidi ya Valencia, Atletico Madrid walikuwa wamekatiza msururu wa Barcelona wa mechi saba bila kushindwa

Gerard Pique
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Barca hawajashindwa kwenye mechi tano za ligi mfululizo wakiwa nyumbani huku wakishinda mara nne na kupata sare moja katika uwanja wao wa kihistoria wa Camp Nou.
 
Wakati huo huo katika mechi iliopita, Madrid wakiwa ugenini walipoteza mchezo wao na Espanyol mabao 2-1 kwenye mchezo wa ligi uliochezwa oktoba 3
 
Kwa sasa, hawajapata ushindi katika mechi mbili zilizopita huku wakiambulia sare moja na kushindwa mara moja.
 
Kufuatia kushindwa na Espanyol, Madrid walishindwa kwa mara ya kwanza ugenini katika michezo 17 ya ligi iliyopita.

Karim Benzema
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
 “Maoni yangu yanabakia pale pale. Ni mechi kubwa Zaidi kwenye historia ya kandanda. Haijalishi wachezaji walioko, walioondoka na watakaokuja. Barcelona dhidi ya Madrid ni mechi ya kihistoria”, alisema mshambuliaji wa Madrid Karim Benzema.
 
 “Zamani kulikuwa na Zinedine Zidane, Ronaldinho, Ronaldo na Samuel Eto’o. Wachezaji watabadilika lakini mechi itabaki ile ile tu, Madrid dhidi ya Barcelona.
 
 
“Hakuna wakati mwafaka wa kucheza dhidi yao. Timu kama Barcelona au timu nyingine kubwa inaweza kuwa na mchezo mmoja mbaya kisha mchezo wao unapaa tena. Ni mchezo mgumu ambao hutuwezi kuchukulia mzaha hata kama wamekuwa na matokeo duni ya hivi karibuni.”
 
Mchezo wa mwisho baina ya timu hizo mbili ulichezwa Aprili 10 2021
Madrid waliibuka washindi 2-1 katika mchezo huo wa kusisimua uliogaragazwa katika uga wa Estadio Alfredo Di Stefano.
 

Takwimu baina ya timu hizi mbili katika mechi tano za mwisho za ligi

Mechi - 5
Barcelona - 2
Madrid - 1
Sare - 1

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway

Published: 10/19/2021