Atletico kukata mbawa za Liverpool


Hakimiliki ya picha: Getty Images


2021/22 UEFA Champions League 

Group B 

Atletico Madrid v Liverpool FC 

Estadio Wanda Metropolitano
Madrid, Spain 
Tuesday, 19 October 2021 
Kick-Off 22h00
 
Oktoba 19 kutakuwa na mechi ya ligi ya mabingwa ulaya Atletico Madrid watakapoialika Liverpool katika mechi ya makundi.
 
Miamba hao wa Uhispania walitoka nyumba na kushinda waliokuwa mabingwa wa Italia 2-1 ugenini katika mechi yao ya mwisho ya kundi B September 28.
 
Atletico wameepuka kushindwa katika mechi mbili za mwisho za UEFA huku wakipata ushindi wa mechi moja na kulazimisha sare moja.

Koke
Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 
 
Hata hivyo, Atletico, maarufu kama watengeneza magodoro hawajapata ushindi katika mechi nne za nyumbani. Wameshindwa mechi moja na kupata sare mechi tatu.
 
Wakati huo huo, Liverpool waliinyuka Fc Porto ya Ureno 5-1 ugenini katika mchezo wao wa kundi B uliochezwa Septemba 28.
 
 
Miamba hawa wa England wameshinda mechi mbili mfululizo na kutoka sare moja kwenye mashindano haya
 
Katika mechi tatu za ugenini, Liverpool wameshinda mechi mbili na kupoteza mchezo mmoja kwenye ligi hii.

Jurgen Klopp
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
“Hatukuanza mechi vizuri kwa sababu ni dhahiri Porto walishuhudia mechi yetu na Brentford hivyo walifahamu jinsi ya kututhibiti,” Alisema mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp baada ya kuishinda Porto.
 
“Tulicheza vizuri dhidi ya timu iliyojituma Zaidi kwa nyakati tofauti hasa ukizingatia walipoteza mlinzi wa kati kwa jeraha kwenye mechi yao na Atletico na mchezaji mwengine akapata jeraha  leo wakati wa kupasha.
 
 
“Ni dhahiri kwa ni vigumu kucheza mchezo mzuri unapowakosa wachezaji muhimu. Hakika, inakuwa mbaya Zaidi unapocheza nasi katika hali hii. Tulitumia masaibu yao kwa manufaa yetu. Tulikuwa na mchezo mzuri sana na kufunga magoli ya kuvutia lakini pia tulitengeneza nafasi nzuri zaidi. Kwa ujumla, ilikuwa jioni nzuri,’.
 
Machi 11 2020 ilikuwa ni siku ya mwisho timu hizi mbili kukutana katika mashindano haya ya UEFA
 
Atletico waliibuka na ushindi wa 3-2 katika mechi hiyo iliyochezewa ugani Anfield, England.
 

Takwimu baina ya timu hizi mbili kwenye ligi ya mabingwa Ulaya

 
Mechi – 4
Atletico - 2
Liverpool - 0
Draws - 2


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

 

Published: 10/18/2021