UHAKIKA HILI: USAJILI MPYA WA YANGA DIRISHA DOGO HUU HAPA


KOCHA mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amependekeza nafasi tatu kuweza kuboresha kipindi cha usajili wa dirisha dogo ambalo linatarajiwa kufunguliwa Desemba mwaka huu.
 
Katika nafasi hizo ni kiungo mshambuliaji ambaye anatajwa Abdoulaye Djire kutoka klabu ya Racing De Abidjan ya Ivory Coast, kiungo mkabaji na mshambuli baada ya Kennedy Musonda, Clement Mzize na Hafiz Konkoni kushindwa kuziba nafasi ya Fiston Mayele.
 
Kocha Gamondi amsema licha ya kikosi chake kuonekana imara lakini kuna nafasi anatakiwa kuboresha na kuongeza nguvu kipindi cha dirisha dogo.
 
“Viongozi wanajua kipi kinahitajika kwa ajili ya timu nimewapa nafasi ya kufanyia kazi lakini tunahitaji watu kuja kutuongezea ubora kwenye mechi ngumu zilizopo mbele yetu ikiwemo michuano ya kimataifa.
 
"Tunapoingia kwenye maboresho kuna mambo ya kuzingatia ni wapi mtapata mtu au watu mnaowahitaji kwa ajili ya kuongeza nguvu ambao wataonyesha ubora zaidi ya waliopo ndani ya kikosi cha sasa,” alisema Kocha huyo na kudai kuwa anataka kuona wanaosajiliwa wanakuwa bora zaidi.
 
Wakati huo huo Ofisa habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema benchi la ufundi limemekabidhi mapendekezo yake ya dirisha dogo na Rais Hersi Saidi kufabyia kazi.
 
Amesema hakutakuwa na maboresho makubwa sana na kuhusu nafasi zipi zitakazosqjiliwa hilo lipo ndani ya uongozi unaosimamia akiwemo Rais Hersi na Mtendaji mkuu Endrew Mtime.
 
“Tayari viongozi wameshaanza kufanyi kazi na itakapofunguliwa dirisha la usajili kazi itakuwa ni kutambulisha wachezaji na sio kuanza kutafuta.
Niwahakikishie wanayanga kuwa tunasajili watu,” amesema Kamwe.
 
Kuhusu maandalizi kuelekea mchezo wao wa kimataifa dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria, Kamwe alisema licha ya nyota wao kuwepo kwenye majukumu ya timu za taifa, waliobakia wanaendelea na majukumu ya klabu.
 
“Maandalizi yanaendelea vizuri na timu inafanya mazoezi kujiandaa na mchezo huo, tunahitaji kwenda Algeria kutafuta matokeo na kuonyesha ukubwa wetu wa kusaka matokeo ugenini,” amesema.

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Bashiri popote
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 11/17/2023