SIMBA SC WAAMUA KUKOMAA NA MOSES PHIRI


KLABU ya  Simba imewaondisha shaka wanachama na mashabiki wa Simba kuhusu straika wao Moses Phiri ikisema hatoenda popote, badala yake atabaki kuwa mchezaji wa timu hiyo na suala  la kutopata nafasi linabaki ni jukumu la Kocha Mkuu Roberto Oliveira (Robertinho).
 
Klabu hiyo imesema hivyo,  baada ya tetesi kuwa nyota huyo anahitaji kuondoka ndani ya klabu hiyo huku akitajwa kutua kwa wapinzani wao Yanga kipindi cha usajili ya dirisha dogo Desemba mwaka huu
 
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Simba, Ahmed Ally alisema Phiri bado ni mali yao na hawafikirii kuachana na nyota huyo ambaye amekuwa akipata nafasi, anafanya vizuri.
 
 
Aliongeza kuwa nyota huyo alikuwa sehemu ya kikosi kilichoingia kambini juzi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga, utakaochezwa, Jumapili  Novemba 5 mwaka huu.
 
 
Simba ni wenyeji  katika mchezo huo wa Darby utakaochezwa jumapili hii, uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, saa 11: 00 jioni.
 
 
Alisema Phiri ataendelea kuwepo kwenye kikosi cha Simba na hakuna kwa klabu Tanzania  ambayo inaweza kumchukuwa kama bado wanahitaji huduma ya nyota huyo.
 
 
“Ni kweli kuna taarifa tunaziona juu ya Phiri, ukweli ni kuwa mchezaji huyo bado ataendelea kubaki ndani ya klabu hiyo, inapofikia kipindi cha usajili utaona Yanga inataja kuchukuwa baadhi ya nyota wetu.
 
 
Suala la kupata nafasi ya kucheza liko chini ya kocha Robertinho, ukizingatia kuna mechi nyingi na tunaimani Phiri au mchezaji yoyote ndani ya Simba watapata nafasi ya kucheza,” alisema Ahmed.
 
 
Kuhusu maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Yanga, Ahmed alisema mipango yao kutafuta alama 15 za awamu ya pili katika michezo mitano iliyopo mbele yao wakiendeleza kutafuta pointi tatu dhidi ya Yanga.
 
 
“Msimu huyu tumegawamu awamu sita katika michezo yetu ya ligi, mechi tano kila awamu tumemaliza awamu ya kwanza kuvuna alama 15, sasa tunaenda hatua ya pili ambayo mechi ya kwanza na Ihefu FC tumemaliza.
 
 
Kazi kubwa ipo mechi nne zilizosalia ikiwemo dhidi ya Yanga, tunahitaji kupata alama tatu muhimu ili kujiweka katika ramani ya dhamira yetu ya msimu huu kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara,” alisema
 
 
Alisisitiza kuwa wameingia kambini mapema jambo sio kawaida yao, kwa mechi za ndani hiingia siku tatu kabla lakini safari hii wameingia siku sita kabla ya kukutana na Yanga.
 
 
“Simba tunahitaji hii mechi na kupambana kuendeleza ubabe wetu kwa muda wote, lazima tuhakikishe tupate ushundi ili kufiki dhamila yetu ya kutwaa ubungwa,” alisema Meneja huyo.
 
 
Aliongeza kuwa wamedhamiria kutwaa ubingwa mapema na kufika huko lazima wamfunge Yanga katika mchezo wao wa jumapili na kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo.
 
 
“Azam FC tayari ameshajitoa katika mbio za ubingwa na kazi iliyosalia kumfunga Yanga,  mechi ya jumapili tumedhamilia kuendeleza ubabe wetu kwa watani wetu, baada ya mchezo wa Ihefu FC tukaanza maandalizi ya mechi na Yanga, Simba tumewekeza nguvu nyingi sana kwa sababu ukipoteza au kushinda basi tutakumbuka milele.
 
 
Hatuwezi kukataa kuwa Yanga wamekuwa na kikosi bora, wachezaji wanapambana, tumefatilia mechi na tunaenda kukutana na mpinzani ambaye yuko fiti,  licha ya ubora wetu lakini tunatakiwa kutafuta ushindi kwa jasho ili kufikia malengo yetu ya kusaka alama tatu katika mechi tano za hatua ya pili,” alisema.
 
 
Aliwaomba mashabiki kuzingatia misingi ya nchini ikiwemi ustaarabu, utu na upendo wanapokuwa uwanjani kwa kutoleta vurugu kwa shabiki mwenzake au mamlaka zilizopo uwanjani.
 
 
Alitaja viingilio vya mchezo huo ni viti vya machungwa ni Shilling 10,000, VIP C 20,000, VIP B 30,000 na A 40,000 huku Platinum 150,000.

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 11/11/2023