MASTAA SIMBA WAPEWA 'LAST CHANCE'...MABOSI WAPISHANA KAMBINI KUYAMALIZA


WACHEZAJI wa Simba wamepewa nafasi ya mwisho kuelekea mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana ili kuonyesha kiwango kwa qjili ya kupigania timu tofauti na hivyo dirisha dogo la usajili litawahusu.
 
Hayo ni maadhimio yaliyofikiwa kati ya viongozi na wachezaji baada ya kikao kizito kilichokaliwa jana usiku baada ya mazoezi katika kambi ya timu hiyo Bweni, kulingana na matokeo na viwango vilivyoonyeshwa katika mchezo dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast majuma yaliyopita uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, kwa kutoka sare ya bao 1-1.
 
Taarifa zilizoifikia kutoka ndani ya klabu hiyo kuwa katika kikao kimejadiliwa mambo mbaLimbaugh ikiwemo matokeo mabaya ya mechi tatu zilizopita pamoja na mikakati kuelekea mechi ijayo dhidi Jwaneng Galaxy, pamoja na ujio wa kocha ambaye utaambatana na usajili wa dirisha dogo.
 
Mtoa habari huyo alisema uongozi umevunja ukimya na wamewaeleza wachezaji juu ya maadhimio yao kuwa hizi mechi mbili za kimataifa zilizopo mbele ni kipimo kwao kuonyesha kiwango kizuri na ikiwa nafasi yao ya kuendelea kusalia ndani ya kikosi hicho.
 
“Kikao cha kwanza kilifanyika juzi baada ya dakika 90 na Asec Mimosas kukamilika viongozi walichukizwa na kuwaeleza kuwa asiyetaka kujituma akamuona Mtendaji mkuu na kumpa barua na haki zake, lakini hilo halikutokea.
 
Lakini jana viongozi waliamua kuibuka kambini na kuzungumza na wachezaji kuweka sawa na kila mmoja wao kujiwekea mikakati yao kuelekea mechi mbili za kimataifa tunazokwenda kucheza ugenini lakini ni nafasi kwa mchezaji kuonyesha kwa sababu ni mechi ambazo zitaamua hatima yake ya kusalia dirisha dogo,” alisema mtoa habari huyo.
 
Aliongeza kuwa hatua hiyo ni baada ya ujio wa Kocha mpya, Abdelhak Benchikha anayetarqjia kutua nchini muda wowote ili kuona timu yake na Alhamisi kuambana na timu hiyo kwenda nchini Botswana.
 
“Tayari kocha amepewa makali yote kuhusu maboresho na atatumia michezo hiyo miwili ikiwemo dhidi ya Jwaneng Gallaxy na Wydad Casablanca ya Morocco. Timu itaondoka na ndege ya kukodi hadi Botswana baada ya mechi kikosi kitaondoka kuelekea Morocco,” alisema mtoa habari huyo.
 
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, alisema kikao kimemliza kila kitu na kuweka sawa mambo yote kazi iliyobaki ni wachezaji kwenda kutafuta matokeo chanya katika mechi mbili zilizopo mbele yetu.

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Bashiri popote
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 11/29/2023