LICHA ya kuanza kuingia sokoni kuanza kuangalia nyota wapya, uongozi wa
Simba umeweka wazi kuwa suala la kuboresha litakuwa chini ya kocha mkuu mpya ambaye wanatarajia kumtangaza ndani ya wiki hii.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, amesema kocha huyo atapewa faili ya wachezaji wote na kuangalia mechi zilizocheza Simba pamoja na kujiridhisha na wachezaji alikuwa nao ambaye hatajituma atapoteza nafasi ndani ya kikodi hicho.
Simba ipo kwenye mchakato wa kutafuta kocha mkuu ambaye anakuja kurithi mikoba ya Roberto Oliviera (Robertinho) huku akitajwa Kocha wa USM Alger ya Algeria, Abdelhak Benchikha na Sven Vandenbroeck amewahi kufundisha Wydad Club Athletic ya Morocco, Vandenbroeck alikuwa kocha wa Simba kwa mafanikio katí ya 2019 na 2021 akiipa mataji mfululizo na kuifikisha Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kabla ya kutimkia FAR Rabat ya Morocco.
Try Again amesema kwa sasa wako kwenye hatua ya mwisho ya kumtambulisha kocha mpya ambaye atakuwa na jukumu kubwa la kufabyq maboresho kipindi cha usajili ya dirisha dogo.
Amesema mara nyingi hutoa nafasi kwa kocha kuangalia machaguo yake ni aina gani ya mchezaji anayemtaka kulingana na mfumo wake lakini pia wanahitaji kuona wachezaji waliopo sasa kujituma.
“Tumewapa mwezi mmoja na nusu nyota kujitathimini kuhakikisha wanajutuma na kuendelea kusalia kikosini ninaimani kuna watopoteza nafasi ndani ya timu.
Bodi yangu na viongozi wengine hatutakuwa tayari kuona sehemu ya kuvumilia kuona mchezaji ambaye hajitumi, Simba inahitaji nyota ambao watatufikisha pale tunapotarajia ikiwemo kutwaa mataji ya ndani na kufanya vizuri zaidi kimataifa ikiwemo kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” almesema Try Again na kusisitiza kuwa :
Kocha anatarajia kuja ni bora na pia ana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika pamoja mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kuhusu majina yanayotajwa sifahamu ila ninachofahamu tunaleta mwalimu wa kututoa hapa kwenye robo fainali na kutupeleka nusu fainali.
Kuhusu kocha Sven Vandenbroeck alikiri ni kocha mzuri lakini amewataka mashabiki kuwa watulivu kuona viongozi kufanya majukumu yao kwa kuleta mwalimu bora zaidi.
Try Again ameongeza kuwa viongozi wa klabu hiyo kuwa kitu kimoja na kushikamana ili Simba ifanikiwe katika mipango yao hasa kuelekea mchezo wao wa wikiendi hii dhidi ya Asec Mimosas.
“Shukrani kwa mashabiki wetu kuendelea kusapoti timu katika hali yoyote, naomba waendelee sapoti hiyo hiyo na pia nawaomba viongozi tuwe pamoja na tukishirikiana hakuna timu yoyote itakayotufunga hapa au kututoa.
Kwa sasa tunatakiwa kusahau kila kitu kilichotokea nyuma katika michezo miwili na sasa nguvu na akili zetu katika mechi yetu ijayo dhidi ya Asec Mimosas,” amesema Try Again.
Kikosi cha Simba chini ya kaimu kocha Daniel Cadena na Selema Matola kwa wachezaji ambao hawako kwenye majukumu ya timu za taifa wanaendelea mazoezi kujiandaa dhidi Asec Mimosas utakaopigwa wikiendi ijayo uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.