EPL - Newcastle United v Arsenal


Hakimiliki ya picha: Getty Images


2023/24 English Premier League
Matchday 11

Newcastle United v Arsenal

St James' Park
Newcastle upon Tyne, England
Saturday, 4 November 2023
 
Newcastle wanapania kukabili matokeo mabaya dhidi ya Arsenal kwenye ligi watakapokutana ugani St James' Park mnamo Jumamosi Novemba 4.
 
The Magpies wamepata ushindi dhidi ya Arsenal mara 11 tu tangu kuanzishwa kwa mfumo mpya wa ligi ya Premier, huku mara mbili kati ya hizo zikija wakiwa nyumbani ndani ya misimu sita iliyopita.
 
Eddie Howe amefanya kazi nzuri kabisa tangu klabu hiyo kuwa chini ya mwenyeji mpya huku akifanikiwa kuipeleke klabu hiyo kwenye shindano la ligi ya mabingwa ulaya kwa vilabu baada ya miaka 20.
 
Newcastle walitoa sare ya 2-2 dhidi ya Wolves ugani Molineux Oktoba 28 na sasa wanashikilia nafasi ya sita kwenye jedwali la ligi. Baada ya kushinda mchezo wa hawamu ya kumi, Tottenham, Arsenal, City, Liverpool na Aston Villa wanashika nafasi ya kwanza, pili, tatu, nne na tano mtawalia.  
 
Baada ya kupoteza mechi zao, Manchester United na West Ham United wanachukua nafasi ya nane na tisa mtawalia wakiwa na alama 17 sawia na Brighton waliopo katika nafasi ya saba.

Callum WilsonHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Arsenal waliendeleza msururu wa matokeo mazuri msimu walipoibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Sheffield United ugani Emirates.
 
Vijana wa Mikel Arteta walikwea hadi nafasi ya pili baada ya ushindi huo mnono ikiwa ni alama mbili nyuma ya wapinzani wao wa jadi Spurs.
 
Callum Wilson anazidi kuonyesha makali yake mbele ya lango la mpinzani baada ya kufunga magoli mawili dhidi ya Wanderers na kufanya kuwa idadi ya magoli matatu katika michezo miwili ya ligi iliyopita. Licha ya kutumika kama mchezaji wa akiba mara nyingi msimu uliopita nyuma ya Alexander Isak, Wilson alifanikiwa kufunga magoli 18 na kusaidia timu hiyo kumaliza katika nafasi ya nne. Kwa sasa anashikilia nafasi ya nne katika orodha ya wafungaji bora msimu huu akiwa na magoli saba ndani ya michezo tisa.  
 
Eddie Nketiah of Arsenal
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Mshambuliaji Eddie Nketiah anaonekana kuzidi kumpa wakati mgumu mkufunzi Arteta kuchagua kikosi chake baada ya kuzidi kupachika magoli zaidi kila anapopata nafasi. Hii ni baada ya kufunga magoli matatu dhidi ya Blades kwenye mechi ya ligi iliyopita. Uchezaji mzuri wake umemuweka mshambuliaji Gabriel Jesus nje ya uwanja msimu huu na amelipa imani ya kocha wake kwa kufunga magoli matano katika michezo kumi hadi sasa.
 
Howe alilalamikia kukosa wachezaji kadhaa katika safu ya ushambuliaji kwenye mechi dhidi ya Wolves. Alifanya badiliko la mchezaji mmoja tu ugani Molineux kwa sababu ya kuwa na walinzi wengi kama wachezaji wa akiba huku Isak na Jacob wakiuguza majereha naye Sandro Tonali akitumikia marufuku ya miezi 10 kwa kuvunja sheria kuhusu kucheza kamari.
 
"Nimebaki na wachezaji wengi wa safu ya ulinzi kuliko washambuliaji,” alisema baada ya mchezo huo. “Sharti niwe makini sana ninapofanya mabadiliko. Yalikuwa maandalizi magumu kufanya kuelekea mchezo huu.
 
"Unahitaji kufanya mabadiliko na kuleta washambuliaji uwanjani ili kupata ushindi lakini hatukuwa nao.”
 
Arteta alisifia sana juhudi za mchezaji Nketiah ambaye alianza mechi yake ya nane msimu huu kwenye mechi dhidi ya Sheffield United.
 
"Nimefurahishwa na juhudi zake,” alisema raia huyo wa Uhispania. Alifunga magoli matatu yaliyohitaji kiwango na utulivu. Hajafunga goli kwa majuma kadhaa lakini leo amepata nafasi, ameonyesha mchezo mzuri na kufunga magoli matatu mazuri kabisa.
 
"Amekuwa akionyesha mchezo mzuri kila wakati na kujituma kwa faida ya timu. Ameshiriki mechi nane za ligi msimu huu. Ni kiashiria cha imani yetu na uchezaji wake na juhudi alizoonyesha.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Newcastle - 1
Arsenal - 3
Sare - 1
 

Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 11:

  
Jumamosi, Novemba 4
 
2:30pm: Fulham v Manchester United
 
5:00pm: Brentford v West Ham United
 
5:00pm: Burnley v Crystal Palace
 
5:00pm: Everton v Brighton & Hove Albion
 
5:00pm: Manchester City v Bournemouth
 
5:00pm: Sheffield United v Wolverhampton Wanderers
 
7:30pm: Newcastle United v Arsenal
 
Jumapili, Novemba 5
 
4:00pm: Nottingham Forest v Aston Villa
 
6:30pm: Luton Town v Liverpool
 
Jumatatu, Novemba 6
 
10:00pm: Tottenham Hotspur v Chelsea

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 11/03/2023