EPL - Chelsea v Manchester City


Hakimiliki ya picha: Getty Images


2023/24 English Premier League
Matchday 12

Chelsea v Manchester City

Stamford Bridge
London, England
Sunday, 12 November 2023
 
Manchester City watakabiliana na Chelsea kwenye mechi ya ligi ugani Stamford Bridge mnamo Jumapili Novemba 12.
 
The Citizens wanaongoza jedwali la ligi kwa alama moja baada ya ushindi wa 6-1 dhidi ya Bournemouth Etihad Stadium Jumamosi iliyopita Novemba 4, huku Arsenal na Tottenham wakipoteza mechi zao za kwanza msimu huu katika mechi za mkondo huo wa 11.
 
The Gunners wanashika nafasi ya 4 kwa sasa baada ya kupoteza mechi mikononi mwa Newcastle kupitia goli la Anthony Gordon lililozua utata mkubwa. Spurs walishuka hadi nafasi ya pili baada ya kichapo cha 4-1 dhidi ya Chelsea Tottenham Hotspur Stadium, mechi waliyocheza na wachezaji tisa baada ya wachezaji wao wawili kuonyeshwa kadi nyekundu.
 
Liverpool wapo katika nafasi ya tatu, alama sawia na Arsenal japo na ubora wa magoli. Hii ni baada ya kutoa sare ya 1-1 dhidi ya Luton ugani Kenilworth Road.

Nicolas Jackson
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Chelsea walitumia nafasi zao vizuri baada Tottenham kupoteza wachezaji wawili na kufunga magoli manne huku Nicolas Jackson akifunga magoli matatu, maarufu kama hat-trick.
 
Timu hiyo ya Mauricio Pochettino ilikwea hadi nafasi ya 10 baada ya ushindi huo ambao ni wa nne msimu huu. Brentford wapo nafasi ya 9, alama moja juu ya Chelsea, Manchester United wanashikilia nafasi ya 8 na Brighton nafasi ya 7.
 
Jackson anayechezea timu ya taifa ya Senegal alijikuta katika nafasi ya nzuri ya kupachika magoli ya kwanza mawili na baadaye kupokea pasi murua, kumchenga kipa wa Tottenham Guglielmo Vicario na kufunga goli lake la tatu. Jackson ni mfungaji bora wa Chelsea msimu huu hadi sasa akiwa na magoli 5 katika mechi 10.

Jeremy DokuAlamy hisa picha
 
 
Jeremy Doku alikuwa na mchango mkubwa katika mechi ya City na Bournemouth. Raia huyo wa Ubelgiji alifunga bao la kwanza la mechi hiyo dakika ya 30 na kuchangia kupatikana kwa magoli mengine manne.
 
Pochettino alifurahishwa na juhudi za Jackson ambaye amekuwa na mwanzo mgumu ugani Stamford Bridge huku akiwa na majukumu ya ziada baada ya majeraha ya Christopher Nkunku.
 
"Nimefurahishwa na juhudi zake. Sote tunafahamu jukumu la mshambuliaji ni kufunga magoli. Wanaumia wasipofunga,” alisema raia huyo wa Argentina. “Ni mchezaji mchanga. Alisajiliwa kipindi cha majira ya joto na sio rahisi kuchezea timu kama Chelsea. Historia yake ni kubwa inayohusu kushinda mataji.
 
"Ni jukumu letu benchi la ufundi kutathmini na kuwasaidia wachezaji na hali wanayohitaji kufanya vizuri. Ni mchezaji anayejiamini sana. Nina furaha magoli hayo yatampa motisha zaidi.”
 
Guardiola amekiri kuwa hufurahishwa Doku anapokuwa na mpira na ameridhishwa jinsi sajili huyo mpya alivyoingiliana na mazingira yake mapya kwa muda mfupi.
 
"Hakuweza kucheza kwa viwango vyake katika mechi ya kwanza dhidi ya Fulham lakini alionyesha uwezo wake kwenye mechi dhidi ya West Ham,” alisema Guardiola. “Alionyesha mchezo mzuri katika mechi hiyo na mechi zote alizocheza uwanja wa nyumbani.
 
"Sio uwezo wa kuwachenga wachezaji tu, ni mchezaji mzuri kwa ujumla. Ametushangaza sisi sote. Ni mchezaji wa kusisimua anapokuwa na mpira. Ananifurahisha pia. Kuna uhakika wa jambo nzuri kutokea.”
 
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Chelsea - 1
Man City - 4
Sare - 0
 

Ratiba ya mechi za Premier League mchezo wa 12:

  
Jumamosi, Novemba 11
 
2:30pm: Wolverhampton Wanderers v Tottenham Hotspur
 
5:00pm: Arsenal v Burnley
 
5:00pm: Crystal Palace v Everton
 
5:00pm: Manchester United v Luton Town
 
7:30pm: Bournemouth v Newcastle United
 
Jumapili, Novemba 12
 
4:00pm: Aston Villa v Fulham
 
4:00pm: Brighton & Hove Albion v Sheffield United
 
4:00pm: Liverpool v Brentford
 
4:00pm: West Ham United v Nottingham Forest
 
6:30pm: Chelsea v Manchester City

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 11/11/2023