Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 FIA Formula One World Championship
2022 Abu Dhabi Grand Prix
Yas Marina Circuit
Abu Dhabi, United Arab Emirates
Sunday, 20 November 2022
Max Verstappen amehapa kumsaidia dereva mwenza wa Red Bull Sergio Perez katika mbio za kukamilisha msimu za
Abu Dhabi Grand Prix Jumapili Novemba 20.
Kulikuwa na kutoelewana baina ya madereva wakati wa mbio za Brazilian Grand Prix wikendi iliyopita baada ya Verstappen kupuuza amri za timu yake kumruhusu Perez kuchukua nafasi ya sita kuelekea mizunguko ya mwisho.
Zilikuwa mbio za kusahau kwa timu ya Red Bull kwani Mercedes walifanikiwa kumaliza katika nafasi ya kwanza na pili kwa mara ya kwanza msimu huu wakifuatiwa na madereva wawili wa Ferrari huku Verstappen na Perez wakichukua nafasi ya sita na saba mtawalia.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kufuatia matokeo hayo, raia huyo wa Mexico anachukua nafasi ya tatu kwenye jedwali la madereva baada ya Charles Leclerc kuzoa alama 290 na kukwea hadi nafasi ya pili, ukizingatia ushindi wake wa mbio 3 dhidi ya mbio mbili.
Verstappen ambaye ni bingwa mtetezi mara mbili wa dunia alijikuta nyuma zaidi kwenye mbio za Sao Paulo baada ya kumgonga Lewis Hamilton wakati wa mzunguko wa saba na kupewa adhabu ya sekunde tano.
Perez alimruhusu dereva mwenza kumpita kwenye mzunguko wa 67 akiwa na matumaini kuwa atarudishiwa nafasi hiyo iwapo Verstappen hatamudu kumpita dereva wa Alphine Fernando Alonso na kuchukua nafasi ya tano.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Licha ya maagizo kutoka kwa mhandisi Gianpiero Lambiase kumruhusu 'Checo' kupita, Verstappen alikaidi huku akimwambia kupitia mitambo ya mawasiliano: “Nilikwambia awali, nyinyi msiniambie hivyo tena.
"Tunaelewana? Nilitoa sababu zangu kuhusu jambo hilo na hazijabadilika.”
Hata hivyo, baadaye Verstappen aliambia kituo cha Sky kuwa: “Tulikaa chini na Sergio, Christian Horner na Helmut Marko na kuwaeleza sababu za kutomruhusu kupita
"Mwisho wa siku unatakiwa kuangalia mbele kutakavyokuwa wakati wote. Iwapo atahitaji msaada kwenye mbio za Abu Dhabi nitamsaidia,”
Matokeo ya mbio za Brazilian Grand Prix 2022
Mshindi: George Russell - Mercedes
Nafasi ya pili: Lewis Hamilton - Mercedes
Nafasi ya tatu: Carlos Sainz - Ferrari
Bashiri Motosport na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni soka, motorsport, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.