Verstappen aotea mafanikio zaidi Sao Paulo


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 FIA Formula One World Championship

2022 Brazilian Grand Prix

Autodromo Jose Carlos Pace
Sao Paulo, Brazil
Sunday, 13 November 2022
 
Dereva wa Red Bull Racing Max Verstappen anatarajia kupata ushindi wake wa 15 msimu huu kwenye mbio za Brazilian Grand Prix Jumapili Novemba 13.
 
Bingwa huyo mtetezi mara mbili aliandikisha rekodi mpya aliposhinda mbio za Mexico City Grand Prix wiki mbili zilizopita huku akivunja rekodi ya ushindi mara 13 iliyoandikishwa na Michael Schumacher, 2004 na Sebastian Vettel, 2013.

Sergio Perez
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Verstappen ana nafasi ya kusawazisha rekodi yake ya ushindi wa mbio tano mfululizo iwapo atashinda mbio za Sao Paulo na Abu Dhabi baada ya kumaliza katika nafasi ya 7 katika mbio za Singapore Grand Prix na kushindwa kuvunja rekodi ya Vettel ya ushindi wa mbio tisa mfululizo mwaka 2013.
 
Vile vile, raia huyo wa Uholanzi anatarajia kumaliza jukwaani mara 18 kama ilivyokuwa msimu uliopita aliposhinda taji la dunia.

Lewis Hamilton
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Verstappen ana lengo na kujenga utamaduni wa ushindi kwenye kampuni ya Red Bull na anatambua kuwa yeye ni mmoja wa timu ambayo juhudi zake zilivunja ubabe wa timu Mercedes kwenye mashindano ya F1.
 
"Tunajaribu kuunda timu nzuri na kutengeneza kumbukumbu pamoja,” dereva huyo mwenye umri wa miaka 25 aliambia tovuti ya Formula 1 website. "Iwapo kanuni na masharti yatabakia kama yalivyo miaka ijayo tutafaidika sana.
 
"Naichukulia Red Bull kama familia yangu ya pili. Walikuwa mabingwa hata kabla sijajiunga nao. Tulipitia kipindi kigumu mwanzoni ila nilizidi kuamini juhudi zetu.
 
"Timu nzima kuanzia walioko kiwandani ina watu wanaoelewa kazi yao. Naamini wana uwezo wa kupata mafanikio makubwa miaka kadhaa ijayo.
 
"Sio jukumu langu kutafuta watu na kujaza nafasi. Hilo liko juu ya uwezo wangu. La muhimu ni kila mmoja kuelewa anachotakiwa kufanya na majukumu yake.
 
"Kampuni ya Honda imeanza kupata huduma za kiwanda chetu cha mfumo wa moto wa gari. Ni vizuri kuelewana jinsi ya kushirikiana kwa pamoja. Ukakamavu mkubwa umeonekana katika kufanikisha kampuni zote mbili kipindi cha miaka michache iliyopita. Tumeweza kupata tulichokuwa tumekosa ili kupigania taji.”
 

Matokeo ya mbio za Mexico City Grand Prix 2022

 
Mshindi: Max Verstappen - Red Bull Racing
Nafasi ya pili: Lewis Hamilton - Mercedes
Nafasi ya tatu: Sergio Perez - Red Bull Racing
 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 
 
 
 

Published: 11/11/2022