Uhispania dhidi ya Ujerumani kupamba Jumapili


Hakimiliki ya picha: Getty Images


Baada ya kupata kichapo kutoka kwa Japan, Ujerumani ina kibarua cha ziada ilhali Uhispania itaelekea kwenye mchezo huo mkali siku ya Jumapili ikiwa na matumaini makubwa.
 
Japan na Costa Rica itaanza siku ya pili ya mchezo katika kundi E ugani Ahmad bin Ali uliopo Al Rayyan.
 
The Samurai Blue ilistaajabisha wengi kwenye shindano hili la mwaka huu walipoibwaga Ujerumani 2-1 katika mechi yao ya ufunguzi siku ya Jumatano.  
 
Die Mannschaft ambayo ni timu ya taifa ya Ujerumani ilipata uongozi kwenye dakika ya 33 kupitia penalti ya mchezaji Ikay Gundogan lakini Japan walitoka nyuma na kushinda mechi hiyo huku magoli ya kipindi cha pili kutoka kwa Ritsu Doan (75') na Takuma Asano (83') yakiwapa vijana Hajime Moriyasu ushindi.  
 
Los Ticos ya Costa Rica itakuwa na kumbukumbu mbaya kutokana na kichapo cha 7-0 kutoka kwa Uhispania siku ya Jumatano, ikikumbukwa pia walipoteza kwa magoli haya hayo dhidi ya Mexico Agosti mwaka 1975.
 
Ubelgiji wanatarajia kuimarisha mchezo wao watakapoikabili Morocco ugani Al Thumama, Doha
 
Vijana wa Roberto Martinez walianza kampeni yao nchini Qatar kwa ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Canada Jumanne, bao lililopachikwa wavuni katika dakika ya 44 kupitia mchezaji Michy Batshuayi.
 
The Red Devils walijitahidi sana katika kipindi cha kwanza kubana mashambulizi ya Maple Leafs huku Martinez akilazimika kufanya mabadiliko mawili baada ya mapumziko ili kupunguza mashambulizi.
 
The Atlas Lions ya Morocco inachukua nafasi ya pili ya kundi F nyuma ya Ubelgiji kwa alama mbili baada ya kutoa sare ya 0-0 dhidi ya Croatia waliomaliza kwenye nafasi ya pili mwaka 2018, Jumatano iliyopita.
 
Timu zote mbili zilikuwa na wakati mgumu kutengeneza nafasi kwenye joto la Al Khor huku matokeo hayo yakifikisha msururu wa mechi sita kwa faida ya Morocco bila kushindwa.
 
Kocha Walid Regragui anahisi alama moja waliyoipata dhidi ya Vatreni inaweza kuwa muhimu sana huku timu hiyo kutoka Magharibi mwa Afrika ikitarajia kuingia hatua ya muondoano kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1986 shindano hilo lilipoandaliwa nchini Mexico.
 
"Unakuwa na wakati mgumu sana unapoanza shindano kwa kupoteza mechi,” alisema Regragui. “Mechi hii inatupa matumaini. Nahisi alama hii ni muhimu sana kwetu.
 
"Hatukufanikiwa kushinda mechi hii lakini matokeo yalikuwa mazuri. Tulijitahidi kadri ya uwezo wetu. Najivunia juhudi za wachezaji hawa. Ilikuwa mechi ya kiwango cha juu sana.”
 
Canada itaelekea kwenye mechi dhidi ya Croatia katika uga wa kimataifa wa Khalifa International Stadium uliopo Al Rayyan baada ya kuonyesha mchezo mzuri dhidi ya Ubelgiji Jumatano.
 
Timu hiyo chini ya mkufunzi John Herdman ilicheza vizuri sana katika kipindi cha kwanza na ilikosa nafasi murua kabisa ya kupata goli la mapema baada ya mkwaju wa penalti wa Alphonso Davies kuokolewa na Thibaut Courtois kunako dakika ya 10.  
 
The Vatreni ya Croatia ilipata wakati mgumu dhidi ya Morocco waliowadhibiti vizuri walipokutana na wanatarajia mechi ngumu hivyo hivyo kutoka kwa taifa hilo na Marekani Kaskazini siku ya Jumapili.
 
Mechi za siku hiyo zitafungwa na Uhispania dhidi ya Ujerumani katika uwanja wa Al Bayt Stadium, Al Khor.
 
La Furia Roja ya Uhispania ilianza michezo hii vizuri sana kwa kuwachapa Costa Rica 7-0 na kuleta msisimko kwenye michezo hii hasa baada ya sare tatu kwenye siku mbili za awali.
 
Uhispania chini ya Luis Enrique ilipata bao la kwanza kupitia mchezaji Dani Olmo dakika ya 11 huku mabao mengine yakifungwa na Marco Asensio (21'), Ferran Torres (31' penalti, 54'), Gavi (74'), Carlos Soler (90') na Alvaro Morata (90+2)
 
Enrique alifurahishwa na uchezaji wa wachezaji wake walioonyesha juhudi nyingi katika kudhibiti Los Ticos ya Costa Rica huku akisifia mchezo wao kwa ujumla ulioshuhudia wafungaji watano tofauti.

Alex TellesHakimiliki ya picha: Getty Images

 
"Soka inakuwa mchezo wa kuvutia unapopata matokeo kama haya,” alisema. “Tulionyesha umakini mkubwa kwenye mchezo huo huku tukizingatia misingi inayounda timu hii kwa miaka mingi. Tulishambulia kwa kasi na wachezaji 17 walioshiriki walionyesha kiwango chao.
 
"Ni timu ya taifa ambayo imekuwa ikifunga magoli mengi katika mashindano yote tunayoshiriki. Pengine hatuna mchezaji aliye na uwezo wa kufunga magoli 30 lakini tunaye Ferran, Dani Olmo, Marco Asensio, Gavi na sina shaka na upatikanaji wa magoli.” 
 
Timu ya Hansi Flick haina nafasi ya kupoteza mechi nyingine kwani matokeo ya namna hiyo yatapelekea timu hiyo kuyaaga mashindano hayo katika hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo ambayo haitakuwa sifa nzuri kwa mabingwa mara nne wa kombe la dunia.
 
Die Mannschaft walishuhudia utetezi wao wa kombe hilo ukivurugwa katika hatua za kwanza za shindano la mwaka 2018, na kocha Hansi Flick anafanya kila juhudi kuhakikisha hilo halitokei tena huku nia yake ikiwa kurekebisha makosa yaliyopelekea kupoteza mechi dhidi ya Japan.
 
"Baada ya kupoteza mechi hii na pia kupoteza alama tuna shinikizo. Hilo halina shaka. Tutajilaumu wenyewe. Tunahuzunika sana,” alisema.
 
"Tulikuwa kwenye mkondo sahihi katika kipindi cha kwanza. Tulimiliki mpira kwa asilimia 78 na tulikuwa na goli moja. Tulipata nafasi nzuri katika kipindi cha pili lakini hatukuzitumia vizuti.
 
"Japan walijituma zaidi yetu leo. Tulifanya makosa ambayo hayaruhisiwi hasa kwenye shindano kama hili la kombe la dunia. Tunastahili kuimarika.”
 

Ratiba ya mechi za kombe la dunia, Jumapili Novemba 27.

 
12:00: Japan v Costa Rica
 
3:00pm: Ubelgiji v Morocco
 
6:00pm: Croatia v Canada
 
9:00pm: Uhispania v Ujerumani
 

Shinda na Kombe la Dunia

Dunia imekusanyika kushuhudia michuano bora zaidi ya soka. Ingia kwenye Droo yetu ya Kila Siku ya Mechi ujishindie TSh 500,000 na ufurahie Free Predictor.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway. 
 

Published: 11/24/2022