Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022-23 National Basketball Association (NBA)
Regular Season
Orlando Magic v Philadelphia 76ers
Amway Center
Orlando, Florida
Saturday 26 November 2022
02:00
The Orlando Magic wanatarajia ushindi dhidi the Philadelphia 76ers timu hizo zitakapokutana kwenye mechi ya ligi ya mpira wa kikapu
National Basketball Association (NBA) katika ukumbi wa Amway Center Orlando, Florida Jumamosi 26 Novemba saa nane asubuhi majira ya Afrika ya kati.
The Magic hawajawa na matokeo mazuri kwenye michezo ya Eastern Conference na sasa wanajipata sehemu za mwisho za jedwali. Hata hivyo, wikendi iliyopita walionyesha mchezo mzuri ugenini dhidi ya Chicago Bulls kwa kushinda 108-107.
“Sijafunga kikapu cha ushindi kama hicho kwa siku nyingi, tangu Machi 2021 nilipochangia ushindi wa Gonzaga,” alisema Jalen Suggs baada ya kufunga kikapu kilichowapa ushindi dhidi ya Bulls. “Ilifurahisha sana.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Inafurahisha sana kuja hapa na wachezaji wenzangu na kufanya vizuri. Tuliyofanikiwa au kufeli mwaka uliopita tumeyasahau, tuliweza kujifunza mengi na kuimarika. Ni faraja kubwa mwaka huu naweza kucheza kwa kujiamini na kufurahia mchezo na wachezaji wenzangu. Ni mwelekeo mzuri kwetu sote. Nahisi tunafuata mkondo mzuri,” aliongeza Suggs.
Kwengineko,The 76ers wapo katikati mwa jedwali kwenye michezo ya Eastern Conference baada ya matokeo mseto hadi kufikia wakati huu wa msimu japokuwa mchezaji Joel Embiid anazidi kuwa na mchengo mkubwa kwenye timu hiyo. Wikendi iliyopita alichangia alama nyingi kwenye mechi dhidi ya Milwaukee Bucks ambapo walipata ushindi wa 110-102.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Anacheza vizuri muda huu,” alisema kocha wa Philadelphia Doc Rivers kuhusu mchezaji Embiid. “Kuelekea mwisho wa mechi kasi ya mchezo ilipungua sana. Tulimpa maelekezo jinsi ya kufanya dakika sita za mwisho na alitekeleza vilivyo.”
Timu hizi mbili zimekutana mara 125 kwenye msimu wa kawaida tangu mwaka 1989-90. Orlando wameshinda mara 79 ukilinganisha na mara 46 kwa faida ya Philadelphia.
Mechi ya mwisho timu hizi zilikutana mnamo Machi 13 2022 ambapo 76ers walipata ushindi wa 116-114 dhidi ya Philadelphia huku Joel Embiid akichangia alama 35. Huu ulikuwa ushindi wa nane mfululizo kwa 76ers dhidi ya Philadelphia.
Takwimu baina ya timu hizi.
Orlando Magic dhidi ya Philadelphia 76ers msimu wa kawaida.
Mechi: 125
Magic: 79
76ers: 46
Ratiba ya mechi za NBA, 26-27 Novemba 2022
Novemba 26 Jumamosi
01:00 Charlotte Hornets v Minnesota Timberwolves
03:00am Orlando Magic v Philadelphia 76ers
03:30am New York Knicks v Portland Trail Blazers
04:00am Indiana Pacers v Brooklyn Nets
04:00am Oklahoma City Thunder v Chicago Bulls
04:00am Miami Heat v Washington Wizards
04:00am Memphis Grizzlies v New Orleans Pelicans
04:00am Milwaukee Bucks v Cleveland Cavaliers
04:00am Houston Rockets v Atlanta Hawks
04:00am Boston Celtics v Sacramento Kings
04:00am San Antonio Spurs v Los Angeles Lakers
05:00am Phoenix Suns v Detroit Pistons
06:00am Golden State Warriors v Utah Jazz
Novemba 27 Jumapili
01:00 Toronto Raptors v Dallas Mavericks
04:00am San Antonio Spurs v Los Angeles Lakers
04:00am Houston Rockets v Oklahoma City Thunder
05:00am Phoenix Suns v Utah Jazz
11:00pm Brooklyn Nets v Portland Trail Blazers
11:30pm Minnesota Timberwolves v Golden State Warriors
12:00pm Los Angeles Clippers v Indiana Pacers
Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.