Gunners na Blues kukutana kwenye dabi ya 206 ya London


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 15

Chelsea v Arsenal

Stamford Bridge
London, England
Sunday, 6 November 2022
Kick-off is at 15h00  
 
Arsenal watakuwa wageni ugani Stamford Bridge kukabiliana na Chelsea kwenye mechi ya ligi Jumapili Novemba 6 wakiwa na nia ya kuzidi kushikilia nafasi ya kwanza kwenye jedwali.  
 
The Gunners wamekuwa wakiongoza ligi hadi kufikia sasa, wakiwa alama mbili mbele ya Manchester city baada ya mechi 12.
 
Vijana wa Mikel Arteta walirudi katika nafasi ya kwanza kwa kuwapiga Nottingham Forest 5-0 jumapili. Hii ni baada ya City kuchukua uongozi wa ligi japo kwa muda mfupi Jumamosi.

Reiss Nelson
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Arteta alifurahishwa na juhudi za wachezaji wake kwenye mechi hiyo baada ya kupoteza 2-0 dhidi ya PSV Eindhoven Alhamisi katika mechi ya Europa ambayo ilifuatia sare ya 1-1 dhidi ya Southampton wikendi iliyopita.
 
"Timu kubwa zinastahili kuonyesha uwezo wao haraka iwezekanavyo baada ya mapungufu na tulifanya hivyo baada ya kupoteza mechi ya Alhamisi,” alisema raia huyo wa Uhispania.
 
"Hakuna muda. Unasafiri Ijumaa jioni. Unakuwa na mazoezi ya muda mfupi na unatakiwa uwe imara kimwili na kiakili kwa ajili ya mechi dhidi ya timu iliyowashinda Liverpool. Kuna shinikizo muda wote.
 
"Sharti tuzoee mazingira na hali kama hii.”
 
The Blues walipoteza mechi ya kwanza chini ya ukufunzi wa Graham Potter baada ya kupata kipigo cha 4-1 dhidi ya timu yake ya zamani Brighton wikendi iliyopita.
 
Potter alikuwa hajapoteza mechi ya ligi katika mechi zake tano za kwanza na Chelsea japokuwa nafasi ya kupigania ubingwa wa ligi ulitiwa dosari na sare mbili zilizofuatiwa na mechi waliyopoteza dhidi ya Brighton.

Kai Havertz
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Raia huyo wa Uingereza alibeba lawama ya matokeo dhidi ya Brighton na kusisitiza kuwa atachambua mchezo huo ili kugundua walichokosea.
 
"Brighton ni timu nzuri na tunafahamu hilo. Walituweka chini ya shinikizo ukizingatia mazingira yaliyotengenezwa na mashabiki wao,” alikiri Potter. “Tulifanya makosa madogo nyakati tofauti za mwanzo wa mechi ambalo ni jambo la kawaida wakati mwingine.
 
"Siwezi kuwalaumu wachezaji hawa kwa matokeo ya mechi hii. Wamekuwa wakicheza vizuri na wamejituma sana. Nachukua lawama za matokeo hayo na nitajaribu kutafuta njia za kurekebisha hali hiyo.
 
"Unastahili kuchambua mchezo na kutambua makosa unapopoteza. Ni sehemu ya kazi yetu. Nachukua lawama iwapo hilo halijatimia na kutafuta mbinu za kuimarisha hali yenyewe.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi

Mechi - 5
Chelsea - 1
Arsenal - 3
Sare - 1
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 11/02/2022