Gunners kukabana koo na Wolves


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 16

Wolverhampton Wanderers v Arsenal

Molineux
Wolverhampton, England
Saturday, 12 November 2022
Kick-off is at 22h45  
 
Arsenal wanatazamia kuingia mapumziko ya kombe la dunia wakiongoza ligi huku wakifukuzia ushindi wa tatu mfululizo dhidi ya Wolves Jumamosi Novemba 12 ugani Molineux.
 
The Gunners walishinda mechi zote mbili za msimu uliopita dhidi ya Wolves; ushindi wa 1-0 ugenini na 2-1 ugani Emirates wiki mbili baadaye.
 
Vijana Mikel Arteta wanazidi kuongoza ligi kwa alama mbili mbele ya Manchester City baada ya kuwashinda Chelsea 1-0 Jumapili iliyopita, bao la ushindi likifungwa na Gabriel dakika 63.

Gabriel JesusHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Arteta alisifia mchezo mzuri ulioonyeshwa na wachezaji wake dhidi ya Chelsea, akiongeza kuwa aliona sifa za uchezaji mzuri huku wakiendelea kuimarika chini ya ukufunzi wake.
 
"Ni hatua nyingine tuliyopiga kuelekea ubora. Kuonyesha kwamba uwezo tunao wa kucheza viwango vya juu dhidi ya wapinzani wazuri. Naamini mchezo huu utawasaidia kujiamini zaidi,” alisema raia huyo wa Uhispania.
 
"Timu yetu ina wachezaji wachanga ila leo tumeonyesha wa timu iliyokomaa. Tulionyesha nia, ujasiri na ari katika hali zote. Tumepiga hatua kama timu na leo tumedhihirisha hilo.”
 
Wolves wamepata kocha mpya, Julen Lopetegui ambaye aliridhi mikoba ya Bruno Lage wikendi iliyopita.
 
Mwanzoni, Lopetegui alikataa kazi ya kuifundisha Wolves alipofutwa kazi na Sevilla mwisho wa mwezi uliopita, akiamua kumuuguza baba yake aliyekuwa mgonjwa.  
 
Hata hivyo, raia huyo wa Uhispania atachukua rasmi mikoba ya timu hiyo baada ya mechi ijayo dhidi ya Arsenal huku jukumu hilo likipewa Steve Davis.

Julen Lopetegui
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Wanderers wameshinda mechi moja kati ya mechi sita walizocheza tangu alipofutwa kazi Lage baada ya kupoteza 2-0 dhidi ya West Ham Oktoba 1.
 
Walipoteza 3-2 dhidi Brighton Jumamosi iliyopita na kuwa mechi ya nne bila ushindi. Davis alielezea kutoridhishwa kwake na matokeo hayo akisisitiza kuwa walistahili kushinda mechi hiyo.  
 
"Nafurahi tulifunga magoli mawili lakini inaumiza sana kuruhusu magoli matatu. Tulikuwa na uwezo wa kuyazuia. Tuliyazungumzia baadaye kwa sababu hatukucheza vizuri hivyo basi kurahisisha mambo kwa wapinzani na kuwapa nafasi ya kutufunga,”
 
"Tulionyesha ukakamavu nyakati tofauti za mechi lakini wakati mwingine hatukuzuia vizuri katika eneo let una vile vile tulifanya maamuzi duni.
 
"Tumeonyesha kuimarika katika mechi tatu au nne zilizopita na tutajifunza kutokana na hali hizo zitakazomsaidia Lopetegui atakachukua kazi hii.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi

Mechi - 5
Wolves - 2
Arsenal - 3
Sare - 0
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 
 

Published: 11/09/2022