Bagnaia aotea taji la kwanza la MotoGP


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 MotoGP World Championship

2022 Valencian Community Grand Prix

Circuit Ricardo Tormo
Cheste, Spain
Sunday, 6 November 2022
 
Mwendeshaji wa timu ya Ducati Lenovo Francesco Bagnaia anahitaji kumaliza katika nafasi ya 13 au juu kwenye mbio za Valencian Community Grand Prix Jumapili ya Novemba 6 ili kutawazwa bingwa wa dunia wa shindano la 2022.
 
Raia huyo wa Italia alipata ushindi wake wa saba wa msimu katika mbio za Malaysian Grand Prix na kukwea alama 23 zaidi ya Fabio Quartararo wa Monster Energy Yamaha kwenye jedwali la waendeshaji huku ikisalia mbio moja msimu kukamilika.

Fabio Quartararo
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Bagnaia hakuweza kutawazwa kwenye mbio za Sepang baada ya Quartararo kumaliza katika nafasi ya tatu kuhakikisha mshindi ataamuliwa na matokeo ya mbio za mwisho.
 
Baada ya kusuasua mwanzoni mwa msimu, mwendeshaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amemarika kwenye nusu ya pili ya mwaka huku akimaliza kwenye nafasi za jukwaani mara nane kati ya mbio tisa.

Enea Bastianini
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kabla ya ushindi wa mbio nne mfululizo kwenye mbio za Dutch Tourist Trophy, Bagnaia alikuwa alama 91 nyuma ya Quartararo na mkurugenzi wa michezo wa Ducati Paolo Ciabatti amewasuta wanaomkosoa mwendeshaji wao kwenye mitandao.
 
"Hilo limemuathiri na kumpa shinikizo Quartararo kufikia kiwango amelazimika kujiondoa kwenye mitandao ya kijamii kwa wiki chache. Inaweza kuwa changamoto kwa mwendeshaji kwamba sio watu wengi wanafurahia anachokifanya lakini unatakiwa kuelewa kwamba ndio maisha ya dunia ya leo na unatakiwa kujifunza kuishi nayo,” Ciabatti aliambia mtandao wa GPOne.
 
"Ukiangalia mbio ambazo Bagnaia ameshinda na mizunguko aliyoongoza, wengi wanaomsema ni kwa sababu ni mashabiki wa waendeshaji wengine au kwa sababu wanamuona Pecco kama Valentino. Hawafanyi vizuri.  
 
"Usipokuwa na mbinu ya kujizuia na jumbe kama hizi za mitandao ya kijamii utapata shinikizo kubwa.
 
"Pecco amefanya vizuri sana na ameonyesha weledi wake. Walio na roho chafu ndio pekee watakaotilia shaka mafanikio yake na hatuna sababu ya kujihusisha na watu kama hao.”  
 

Matokeo ya mbio za Malaysian Grand Prix 2022

 
Mshindi: Francesco Bagnaia - Ducati Lenovo Team
Nafasi ya pili: Enea Bastianini - Gresini Racing
Nafasi ya tatu: Fabio Quartararo - Monster Energy Yamaha
 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 

Published: 11/04/2022