Hakimiliki ya picha: Getty Images
Argentina na Ufaransa ambayo ni mojawapo ya mataifa yanayopigiwa upatu
kushinda shindano la kombe la dunia wataanza kampeni zao Novemba 22.
Argentina ambao ni mabingwa mara mbili wa kombe hilo watafungua kundi C dhidi ya Saudi Arabia ugani Lusail.
La Albiceleste wanaelekea Qatar ikiwa ni mechi 35 bila kushindwa tangu mwaka 2019 kwenye shindano la Copa America waliposhindwa 2-0 na Brazil hatua ya nusu fainali ya shindano hilo.
Lionel Messi ambaye alikuwa nahodha waliposhinda taji la Copa America mwaka 2021 amekisihi kikosi chake kupuuza maneno ya watu na kumakinikia jukumu lililoko mbele yao.
"Ni vigumu kucheza na timu yoyote ya taifa siku hizi,” Messi aliambia Universo Valdano. “Itakuwa changomoto kucheza dhidi ya timu yoyote kwenye shindano la kombe la dunia.
"Hatucheza dhidi ya mataifa ya Ulaya kwenye msururu wetu wa kutokushindwa japokuwa wao hawapendi kucheza dhidi yetu vile vile. Sio rahisi kukabili mataifa kutoka Kusini mwa Amerika.
"Tuko katika hali nzuri kuelekea shindano hili lakini hatuwezi kuamini maneno ya watu kwamba tutashinda shindaono hili. Ni sharti tupambane hatua kwa hatua.”
The Green Falcons, ambayo ni timu ya taifa ya Saudi Arabia wanapania kufika hatua ya muondoano kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994 baada ya kufeli kufanya hivyo katika mashindano manne waliyoshiriki.
Timu hiyo iliyo chini ya Herve Renard imeshiriki mechi kadhaa za kirafiki tangu walipofuzu kushiriki shindano la kombe la dunia na kupoteza mechi ya kwanza dhidi ya Croatia Novemba 16 baada ya mechi saba bila kushindwa.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Denmark na Tunisia watapambana ugani Education City Stadium uliopa Al Rayyan, huku timu hizo mbili zikitarajia kuwashinikiza wapinzani wao katika kundi D.
Timu ya Denmark ina imani ya kufuzu kutoka kundi lao hasa baada ya kuishinda Ufaransa mara mbili katika ligi ya UEFA Nations League.
The Eagles of Carthage, kama inavyojulikana timu ya taifa ya Tunisia haijafuzu kutoka hatua ya makundi baada ya kujaribu mara tano japokuwa wapo katika hali nzuri huku wakipoteza mara moja katika mechi sita walizocheza tangu kufuzu shindano hili kupitia mchujo.
Mexico itacheza dhidi ya Poland ugani Stadium 974 mjini Doha katika mechi muhimu ya kundi C inayotarajiwa kuamua atakayefuzu kuingia hatua ya muondoano.
El Tri wamefanikiwa kuingia hatua ya muondoano katika mshindano saba ya shindano hili yaliyopita ila wamekuwa na matokeo mseto tangu walipofuzu shindano la mwaka huu huku wakiandikisha ushindi mara nne, sare tatu na kushindwa katika mechi tatu.
The Eagles hawajafuzu kutoka hatua ya makundi tangu milenia hii kuanza japokuwa walifanikiwa kushinda mechi moja katika mashindano ya mwaka 2002, 2006 na 2018.
Matokeo yao ya hivi majuzi yamekuwa duni kwa vijana wa Czeslaw Michniewicz wamefanikiwa kushinda mechi mbili tu kati ya mechi sita za UEFA Nations League na kumaliza katika nafasi ya tatu ya kundi 4.
Mabingwa watetezi Ufaransa wanatarajia kuwa na mwanzo mzuri katika shindano hili watakapocheza dhidi ya Australia ugani Al Janoub, Al Wakrah.
Les Bleus wanataka kuepuka yaliyotokea katika shindano la mwaka 2002 ambapo hawakushinda mechi hata moja na kulazimika kuaga mashindano katika hatua ya makundi wakiwa mabingwa watetezi.
Timu hiyo ya Didier Deschamps alianza utetezi wake wa shindano la UEFA Nations League vibaya huku wakipoteza mechi tatu kati ya sita za kundi 1 na kumaliza kwenye nafasi ya 3, nyuma ya Denmark.
Deschamps amelalamikia ukosefu wa muda wa kutosha wa kujiandaa kwa ajili ya mechi ya ufunguzi ya kundi D.
"Wiki moja haitoshi kujiandaa. Ukitazama vizuri utagundua kuna wachezaji wengi waliokuwa wakicheza jana,” alisema.
"Siku mbili tulizonazo; leo na kesho tutatumia kupumzika. Tutasafiri Jumatano na kisha tutakuwa na wiki moja ya kujiandaa kwa ajili ya mechi ya Jumanne kama inavyokuwa kwenye soka ya klabu.”
The Socceroos ya Australia wameshiriki mashindano manne yaliyopita lakini hawajafanikiwa kutoka hatua ya makundi tangu mwaka 2006 walipobanduliwa katika hatua ya muondoano.
Timu hiyo ya Graham Arnold ililazimika kucheza mechi za mchujo ili kufuzu shindano la mwaka huu na kuwabandua Peru na walishinda mechi mbili mfululizo dhidi ya New Zealand hivi karibuni.
Ratiba ya mechi za kombe la dunia, Jumanne Novemba 22.
12:00: Argentina v Saudi Arabia
3:00pm: Denmark v Tunisia
6:00pm: Mexico v Poland
9:00pm: Ufaransa v Australia
Shinda na Kombe la Dunia
Dunia imekusanyika kushuhudia michuano bora zaidi ya soka. Ingia kwenye Droo yetu ya Kila Siku ya Mechi ujishindie TSh 500,000 na ufurahie Free Predictor.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.