Wachezaji 10 wakutazama chini ya miaka 25 kwenye Ligi ya Mabingwa


Hakimiliki ya picha: Getty Images


Wachezaji 10 wakutazama chini ya miaka 25 kwenye Ligi ya Mabingwa
 
Ligi ya Mabingwa imerejea kwa mechi kali hatua ya makundi. Huku timu 32 kutoka ligi bora zaidi barani Ulaya zikiwania taji za Ligi ya Mabingwa, moja ya msimu bora zaidi.
 
Leo, tuangalie wachezaji 10 walio chini ya miaka 25. Ambao watawasha moto na majina yao yataimbwa katika Ligi ya Mabingwa.
 
10. Dominik Szoboszlai
 
Kiungo wa Hungary mwenye umri wa miaka 20 anapambana kutengeneza jina lake kwenye Ligi ya Mabingwa. Dominik Szoboszlai amejiunga na RB Leipzig kutoka RB Salzburg, timu ambayo ni maarufu kwa kuzalisha nyota wa baadaye.
 
Szoboszlai tayari amevutia wengi msimu huu akiifungia timu yake mpya mabao mengi. Anatazamia kufunga jumla ya mabao manne kwenye Ligi ya Mabingwa, ambayo alifunga katika hatua ya makundi msimu uliopita kwa klabu yake ya awali.
 
9. Mason Mount
 
Mwingereza huyo amekuwa na kiwango bora na Chelsea, akitoa fomu nzuri kwa The Blues wakitwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa baada ya kuifunga Man City ya Pep 1-0. Sio tu kwamba alitoa pasi ya mabao kwa Kai Havertz, lakini pia alikuwa na kiwango bora katika mechi ya England dhidi ya Italia katika fainali ya kombe la Ulaya.
 
Ushirikiano wake na Mbelgiji, Romelu Lukaku, utakuwa mzuri sana msimu huu wa Ligi ya Mabingwa.
 
8. Jude Bellingham
 
Jude Bellingham hivi majuzi ameongezwa kwenye orodha ya wanaowania Golden Boy 2021 pamoja na mwingereza mwenzake Mason Greenwood na Bukayo Saka, tuzo iliyonyakuliwa na mchezaji bora chini ya umri wa miaka 21 katika ligi kuu za Ulaya.
 
Kufuatia usajili wake uliyoweka rekodi kutoka Birmingham City kwenda Borussia Dortmund, Jude Bellingham ameendelea kujizolea umaarufu na kuzivutia klabu kubwa barani Ulaya. Ingawa Dortmund haitarajiwi kuletea ushindani katika taji hilo, kikosi chao chenye vijana wenye vipaji kina uhakika wa kutoa mechi kali na timu bora zaidi barani Ulaya..
 
7. Jamal Musiala
 
Musiala anatarajiwa kuwa mchezaji bora katika safu ya ushambuliaji ya Bavaria pamoja na mshambuliaji bora Duniani Robert Lewandowski.
 
 
6. Sandro Tonali
 
Hatimaye AC Milan imerejea kwenye hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa na Sandro Tonali ni mmoja ya vijana wenye kipaji kikubwa uwanjani kwenye kikosi cha miamba hiyo ya  Serie A, ambao wanatazamia kurejea kwa mafanikio kwenye mashindano ambayo wana historia yenye mafanikio.
 
5. Christopher Nkunku
 
RB Leipzig walipoteza wachezaji wao wawili katika dirisha la usajili majira wa joto lakini Nkunku anaendelea kuwa mshambuliaji mkali katika Bundesliga.
 
Licha ya kupoteza dhidi Man City, Nkunku alifunga hat-trick, akionyesha uwezo wake wa kupachika mabao.
 
4. Eduardo Camavinga
 
Camavinga ni kijana mwenye kipaji ambaye alisajiliwa na Los Blancos kutoka klabu ya Stade Rennes ya Ufaransa, hatua ambayo inaonekana kuwa uwekezaji wa muda mrefu.
 
Ingawa Madrid hawakuweza kupata huduma za Kylian Mbappe, mchezaji wa kiwango cha Camavinga anaweza kumvutia Mbappe ikiwa Madrid inaweza kuongeza kwenye orodha ya vijana wenye vipaji.
 
3. Federico Chiesa
 
Nyota huyu wa Italia hivi karibuni ametwaa tuzo ya MVP ya Serie A kufuatia msimu bora 2020/21. Umahiri wake wa kufunga na ustadi wake kwenye mpira unalingana na kasi yake ya kufanya kazi bila kuchoka.
 
Ushujaa wake kwenye michuano ya Euro kwa Italia imefanya kuwa na msimu bora akiwa Juventus, ambao wanapambana kurejea kwenye ubora wako katika ligi na michuano ya Ulaya.
 
2. Kylian Mbappe
 
Mchezaji wa kimataifa wa Ufarasna hakuna ubishi ni moja ya vipaji bora zaidi Duniani kwa sasa. Msimu huu labda ni moja ya nafasi zake bora zaidi za kucheza Ligi ya Mabingwa, huku kuongezwa kwa mchezaji bora wa wakati wote, Lionel Messi, kuongezwa kwenye safu yao ya ushambuliaji majira ya joto.
 
Licha ya tetesi nyingi za uhamisho kumhusisha na Real Madrid, PSG imeongeza wachezaji wa kiwango cha dunia kwenye orodha yao, jambo ambalo linaweza kubadili mawazo yake kuhusu kuondoka Parc Des Princes.
 
1. Erling Haaland
 
Licha ya kuwa na umri wa miaka 21 pekee, Mnorwe huyo tayari amevunja rekodi mbalimbali na kufunga mabao katika Bundesliga na Ligi ya Mabingwa kwa viwango vya kushangaza. Ingawa Dortmund sio miongoni mwa wanaopewa nafasi ya kutwaa taji hilo, ubora wa Haaland unaendelea kuongezeka kila wakati anapoingia uwanjani, na kuvutia vilabu vikubwa zaidi ulimwenguni.
 
Msimu huu, atajaribu kufunga mabao mengi na kudhihirisha kama mshambuliaji hatari zaidi Ulaya.


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 11/05/2021