Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Spanish La Liga
Matchday 15
Villarreal CF v FC Barcelona
Estadio de la Cerámica
Villarreal, Spain
Saturday, 27 November 2021
Kick-off is at 23h00
Villarreal CF na Barcelona watakutana Novemba 27 katika mechi ya
ligi kuu ya Uhispania ugani Estadio de la Cerámica.
The Yellow Submarine, kama wanavyofahamika Villarreal, walitoka sare ya 1-1 na Celta Vigo katika mechi ya ligi iloyochezwa Novemba 20.
Katika michezo miwili ya mwisho ya ligi, Villarreal imeandikisha ushindi mara moja na sare moja.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Vile vile, Villarreal hawajashindwa katika mechi mbili za ligi za mwisho wakiwa nyumbani huku wakipata ushindi mara moja na kutoa sare moja.
“Nakipongeza kikosi hiki kwa kujituma sana hasa wachezaji ambao hawajapata nafasi ya kucheza mara kwa mara,” alisema Unai Emery, meneja wa Villarreal baada ya sare hiyo na Celta
"Ni motisha kwa wachezaji inayowapa msukumo wa kupata ushindi. Tunafahamu fika hatukucheza mchezo mzuri na ni ishara kwamba kuna nafasi ya kuimarika. Mechi ikiwa 1-0, chochote kinaweza kubadilisha matokeo ya mchezo.
"Tulifaa kufunga magoli zaidi, pengine 2-0. Hata hivyo, nafurahi jinsi tulivyocheza mchezo kwa ujumla na pia uchezaji wa wachezaji binafsi kama vile Iborra na Ruben Pena. Sasa tutajipanga kuhusu mechi ijayo na jinsi ya kuimarisha matokeo.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwingineko, Barcelona wakiwa nyumbani waliichapa Espanyol 1-0 katika mechi ya ligi iliyochezwa Novemba 20.
Matokeo hayo yanafikisha kikomo cha matokeo mabaya ya Barca katika mechi nne zilizopita walizoandikisha sare mbili mfululizo na kushindwa mara mbili mfululizo.
Ugenini, Barcelona wamekuwa na matokeo mseto. Hawajapata ushindi katika mechi tano zilizopita za ligi. Wameshindwa mara mbili na kulazimisha sare tatu.
Mechi ya mwisho ya ligi baina ya Villarreal na Barcelona ilichezwa Aprili 25 2021.
Mechi hiyo ilichezewa ugani Estadio de la Cerámica ambapo Barcelona waliibuka na ushindi wa 2-1.
Twakwimu baina ya timu hizi mbili katika mechi tano za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Villarreal - 0
Barcelona - 4
Sare - 1
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.