Michuano bora zaidi ya vilabu Ulaya inaendelea wakati timu 32 zikichuana kuwania nafasi ya kuelekea Urusi Mei 28. Kurejea kwa mashabiki uwanjani kumeongeza morali za timu nyingi zimewakaribisha kwa bashasha.
Kuna baadhi ya mechi kali katika hatua ya makundi na tayari nyingine zimepigwa katika kundi B linaloitwa kundi la kifo, vilabu kama Mabingwa wa Hispania Atletico Madrid, kurejea kwa miamba ya Italia AC Milan na Liverpool. Kwasasa Man City na PSG, vilabu viwili tajiri zaidi kwenye michuano, watachuana kwenye kundi A.
Tunaangalia timu tano za kutazama zaidi kwenye
Ligi ya Mabingwa UEFA tunapoingia katika mojawapo ya misimu ya kusisimua katika soka la Ulaya.
Atalanta
Ikiwa unataka kuweka ubashiri kwa farasi mweusi ambaye anaweza kufika fainali, Atalanta inaweza kuwa timu mojawapo. Kikosi cha Gian Gasperini kimekuwa moja ya kikosi kilichoboreshwa zaidi Ulaya na Italia katika misimu michache iliyopita, mafanikio yao ni kutokana na uchezaji usio na woga, wa kushambulia muda wote. Miamba hiyo ya Italia imejiimarisha kuleta upinzani halisi katika michuano hiyo.
Kutoka timu ya kawaida na ya chini hadi kumaliza nafasi ya tatu ndani ya misimu mitatu iliyopita ya Serie A, Atalanta ni mpinzani mkubwa ambaye ana uhakika wa kutikisa msimu huu.
Manchester United
Cristiano Ronaldo amerejea tena Manchester kwa uhamisho wa kushtukiza kutoka Juventus majira ya joto, Baada ya tetesi kumhusisha na majirani zao Manchester City.
Mashetani Wekundu wamemuongeza Rafael Varane kutoka Real Madrid na Jadon Sancho kutoka Borussia Dortmund kwenye safari yao, kipande ambacho wamekuwa wakitafuta kuongeza kwa fumbo lao kwa muda mrefu.
Mashetani Wekundu hawajashinda taji la Ligi ya Mabingwa tangu Ronaldo aondoke, huku miamba hiyo wa Uingereza ikihangaika kurejea kwenye kiwango baada ya msururu wa makocha.
Ole Gunnar Solskjaer anaendelea kutofautiana maoni ya wadadisi wengi wakihoji kuwa Mnorwe huyo asiye na uzoefu hana kile kinachohitajika kuwaongoza Mashetani Wekundu kutwaa mataji ya nyumbani, achilia mbali Ligi ya Mabingwa. Je, anaweza kuthibitisha wakosoaji kuwa wamekosea?
Atletico Madrid
Atletico Madrid polepole wanajitanabaisha kama moja ya timu ngumu zaidi kuzikabili Ulaya. Mabingwa wa tetezi wa Ligi ya Hispania si wageni kwenye michuano hii, wamefika fainali ya Ligi ya Mabingwa mara mbili na kushinda taji la Europa mara mbili.
Msimu huu, Atletico wameimarisha timu yao kwa kusajili wachezaji kadhaa, maarufu zaidi ni kurejea kwa Antoine Griezmann kwa mkopo kutoka Barcelona.
Chelsea
Kumekuwa na bingwa moja aliyetwaa mara tatu mfululizo katika enzi hizi Ligi ya Mabingwa, ambaye ni Real Madrid imeshinda mara tatu kuanzia 2016 hadi 2018. Chelsea itahitaji kushinda mataji mfululizo chini ya Thomas Tuchel, ambaye alishinda taji hilo baada ya kuinoa Chelsea kwa miezi sita tu.
Tangu aingie uwanjani, mkufunzi huyo wa Kijerumani ameimarisha safu ya ulinzi ya Chelsea, na kuwafanya kuwa wagumu kufungika na kuipa timu hiyo sifa ya kutwaa ubingwa..
Paris Saint-Germain
PSG wamekuwa na dirisha kubwa la usajili majira ya kiangazi wameongeza wachezaji muhimu kwenye kikosi chao ambacho tayari kinavutia. Ongezeko la Lionel Messi, Sergio Ramos, Gianluigi Donnarumma na Achraf Hakimi limekuwa la kuvutia macho kuliko uwanjani.
Paris sio tu waliweza kuimarisha safu yao ya ushambuliaji lakini pia walifanikiwa kuzuia nia ya Real Madrid kupata huduma ya Kylian Mbappe, mchezaji muhimu ambaye angeweza kuwa msaada katika harakati zao za kuwania ubingwa wa Ligi ya Mabingwa. Kwenye karatasi, PSG wanaonekana bora zaidi, lakini wanaweza kutafsiri hili uwanjani hadi msimu huu?
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.