Memphis Grizzlies wataialika Phoenix


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

Memphis Grizzlies v Phoenix Suns

2021-22 NBA Regular Season

Saturday 13 November 2021
FedExForum, Memphis, Tennessee
Tip-off at 04:00 
 
Jumamosi ya Novemba 13 2021, Memphis Grizzlies wataialika Phoenix Suns kwenye mechi ya NBA msimu wa kawaida katika uwanja wa FedExForum ulioko Memphis Tennessee. Mechi inatarajiwa kuanza saa tisa asubui majira ya Afrika ya kati. 
 
Wiki iliyopita, The Grizzlies walishinda mechi mfululizo kabla ya msururu huo kuvunjwa na Washington Wizards wakiwa ugenini, waliowashinda kwa alama 115-87 wikendi iliyopita. “Wanastahili pongezi sana,” kocha wa Grazzlies Taylor Jenkins alisema.

Devin Booker
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Tatizo kubwa kwa Memphis ilikuwa kuwathibiti wachezaji mahiri wa Wizards kama vile Bradley Beal na Montreal Harrel; jambo ambalo Ziaire Williams wa Grazzlies tayari ameshaligundua na wapo tayari kulitatua kabla ya kukabili timu ya Phoenix. 
 
“Bidii ni muhimu sana na ujumlishe hilo na udhabiti tunapowakabili wafungaji mahiri,” alieleza. 
 
Baada ya kusuasua mwanzoni mwa ligi, The Suns wamejikakamua na sasa wanapata matokeo mazuri ikiwa ni pamoja na ushindi wa 123-111 dhidi ya timu nzuri ya Houston Rockets wikendi iliyopita. Ushindi huo ulitiwa dosari na malalamiko ya ubaguzi wa rangi yanayosemekana kuwa yalitolewa na mmiliki wa timu hiyo Robert Sarver na tayari bodi ya ligi ya NBA inafanya uchunguzi. 

Steven Adams
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
"Kuna mambo mengi ya kujadili na kuwaza,” alisema mkufunzi Monty Williams. “Kuna mambo mengi ambayo hayapo wazi tukizingatia ukweli. Mimi kama mmoja wa wahusika wakuu, tuhuma hizi ni kubwa mno. Nakosa maneno ya kuelezea hali hii.” 
 
Anawaasa wachezaji wake kusahau mambo ya nje ya uwanja na kuzingatia mchezo. “Maisha yako katika mchezo yatakuwa mafupi iwapo huwezi kuzingatia mchezo na kusahau mambo yasiyo na manufaa.” 
 
Kuanzia msimu wa 1995/96, Grazzlies na Suns wamekutana mara 95 katika msimu wa kawaida. Phoenix Suns wameshinda mara 57 ukilinganisha na mara 38 kwa faida ya Memphis Grazzlies. Mara ya mwisho kukutana katika msimu wa kawaida ilikuwa Machi 2021 ambapo The Suns walishinda wakiwa nyumbani kwa alama 122-99 dhidi ya the Grazzlies huku Devin Booker akiipatia timu hiyo alama 27 binafsi.
 

Takwimu baina ya timu hizi katika msimu wa kawaida

Games: 95
Grizzlies: 38
Suns: 57
 
 

Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.




Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 11/12/2021