Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021 MotoGP World Championship Season
Valencian MotoGP
Round 18
Circuit Ricardo Tormo
Valencia, Spain
Sunday, 14 November 2021
Mbio za pikipiki maarufu kama MotoGP za Valencia 2021 zitang’oa nanga mwezi Novemba tarehe 14 Valencia Uhispania. Mbio hizo pia zinaitwa The Valencian Community Motorcycle Grand Prix.
Huu utakuwa ni msururu wa kumi na nane na wa mwisho wa msimu wa 2021 wa mbio hizo, na zitafanyika katika mkondo wa Ricardo Tormo.
Mkondo huu ulipewa jina hilo kwa heshima ya mhispania na bingwa mara mbili wa dunia wa mashindano haya Ricardo Tormo aliyefariki mwaka 1998 kwa saratani ya damu, Leukemia.
Mbio za mwaka jana za Valencia zilishindwa na Franco Morbidelli wa Yamaha, Jack Miller wa Ducati alikuwa katika nafasi ya pili huku Pol Espargaro wa KTM akihitimisha nafasi ya tatu bora.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Mbio za hivi maajuzi za mwaka 2021 zilikuwa Alrgave MotoGP ambazo ziliandaliwa Novemba 7.
Francesco Bagnaia wa Ducati alishinda mbio hizo, akifuatiwa na Joan Mir wa Suzuki na Miller akachukua nafasi ya tatu mtawalia.
Bingwa wa mbio hizi wa 2021 Quartararo anaongoza katika jedwali la madereva kwa ujumla akiwa amejizolea alama 267.
Bagnaia yupo nafasi ya pili kwa alama 277 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mir akiwa na alama 195 katika jedwali la madereva mashindano yakielekea ukingoni.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Bingwa mara sita wa mbio za MotoGP Marc Marquez ambaye ni muwakilishi wa timu ya Respol Honda hatashiriki mbio za Valencia kutokana na matatizo ya kuona.
"Baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika kliniki ya Dexeus mjini Barcelona Jumanne iliyopita baada ya ajali akiwa mazoezini, Marc Marquez yupo mapumzikoni nyumbani kwake Cervera,” ilisemekana.
"Akiwa mapumzikoni, ameendelea kujihisi vibaya na kuwa na matatizo ya kuona. Jumatatu alitembelewa na daktari wa macho DR. Sanchez Dalmau katika hospitali huko Barcelona. Baada ya kufanya vipimo, iligundulika kuwa anaugua Diplopia,” iliongeza.
Kwa ujumla, kampuni ya Ducati inaongoza kwenye jedwali, ikifuatiwa na Yamaha katika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Suzuki.
Washindi wa mbio za pikipiki za Valencia 2020
Mshindi: Franco Morbidelli - Yamaha
Nafasi ya pili: Jack Miller - Ducati
Nafasi ya tatu: Pol Espargaro - KTM
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni
soka,
motorsport,
mpira wa kikapu,
rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.