Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021 FIA Formula One World Championship
2021 Qatar Grand Prix
Losail International Circuit
Lusail, Qatar
Sunday, 21 November 2021
Kwa mara ya kwanza,
Qatar itakuwa mwenyeji wa mbio za langalanga zitakazo andaliwa Novemba 21 katika mji wa Lusail.
Huu utakuwa msururu wa ishirini wa msimu wa 2021 wa mbio za langalanga na utaandaliwa kwenye mkondo wa kimataifa wa Losail.
Hii itakuwa mara ya nne mbio hizo kuandaliwa majira ya usiku katika kalenda ya Formula One baada ya mbio za Singapore, Bahrain na Sakhir.
Mbio za hivi karibuni za msimu huu ziliandaliwa Novemba 14 kule Brazil ambapo Lewis Hamilton aliibuka na ushindi.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Nafasi ya pili ilitwaliwa na Max Verstappen wa Red Bull Racing-Honda kisha Valtter Bottas wa Mercedes akamaliza katika nafasi ya tatu katika mbio hizo za Brazil.
Katika jedwali la 2021 la madereva, Verstappen bado anaongoza kwa kuzoa alama 332.5 zikiwa zimesalia mbio tatu msimu kumalizika.
Hamilton akiwa na alama 318.5 na Bottas akiwa na alama 203 wote wa Mercedes wanachukua nafasi ya pili na tatu mtawalia kwenye jedwali la madereva.
Mwendesha-mwenza wa Verstappen katika kampuni ya Red Bull Racing-Honda, Perez anashikilia nafasi ya nne katika jedwali kwa alama 178.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Niliendesha vizuri katika mzunguko wa kwanza,” alisema Charles Leclerc wa Ferrari ambaye anashikilia nafasi ya sita katika msimamo baada ya kumaliza katika nafasi ya tano kule Brazil.
“Kumaliza katika nafsi ya tano yalikuwa mafanikio kwangu. Nafurahi sana. Tulikuwa na kasi nzuri kuliko hata wapinzani wetu wa karibu McLaren-Mercedes.
"Ni ishara kwamba tunazidi kuimarika kwa sababu tuliongeza alama nyingi tu katika msimamo wa ujumla tulipomaliza katika nafasi ya tano na sita.”
Kwa ujumla, kampuni ya Mercedes inaongoza kwenye chati wakifuatiwa na Red Bull Racing-Honda na Ferrari wanafunga nafasi ya tatu bora.
Matokeo ya mbio za langalanga za 2021 za Brazil
Winner: Lewis Hamilton - Mercedes
Nafasi ya pili: Max Verstappen - Red Bull Racing-Honda
Nafasi ya tatu: Valtteri Bottas - Mercedes
Bashiri Motosport na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni soka, motorsport, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.