Mashindano ya gofu ya Houston Open 2021 kung’oa nanga.


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021 Hewlett Packard Enterprise Houston Open

US PGA Tour  

Memorial Park Municipal Golf Course 
Harris County, Texas, USA 
111-14 November 2021
 
Mashindano ya gofu ya Houston Open mwaka 2021 yanatarajiwa kuchezwa kati ya Novemba 11 na 14 kule Harris katika jimbo la Texas nchini marekani. 
 
Ni mashindano ya PGA yaliyoasisiwa mwaka 1946. Mashindano ya 2021 yatadhaminiwa na kampuni ya teknolojia ya Marekani iitwayo Hewlett Packard Enterprise. 
 
Mchezo utafanyika katika bustani la makumbusho la Memorial Park Golf Course ambalo ni moja kati ya maeneo mazuri ya kuchezea gofu nchini Marekani na mashabiki zaidi ya elfu sitini uhudhuria kila mwaka. 

Brooks Koepka
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Carlos Ortiz wa Mexico ndiye bingwa mtetezi baada ya kushinda mashindano ya mwaka jana na ataelekea Houston kutetea taji lake la PGA ambao ni moja kati ya miji yenye mikondo mirefu ya gofu. 
 
Katika mashindano ya mwaka huu ya Hewlett Packard Enterprise Houston Open, Ortiz atapambana na baadhi ya wachezaji bora wa mchezo wa gofu. 
 
Baadhi ya wachezaji hao ni pamoja na Brooks Koepka, Jimmy Walker, Gary Woodland, Patrick Reed, Shane Lowry, Francesco Molinari, Henrik Stenson, Danny Willet bila kumsahau Jason Day. 
 
Mashindano yatahusisha wachezaji 132 ya yatachezwa kwa muda wa siku nne. Washindi wa zamani wa Houston Open Lanto Griffin na Jim Herman watahusika. 

Jimmy Walker
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
“Tunafurahi kuungana na Hewlett Packard Enterprise ili kusaidia wakfu wa gofu wa Astros unaoleta maendeleo katika jamii ya Houston,” alisema rais wa PGA Tour Tyler Dennis..
 
“Houston Open imetengeneza historia tangu 1946 na kufanyika kwake katika bustani la Memorial Park Golf Course kuanzia mwaka jana ni kiashiria kwamba mashindano ya Hewlett Packard Enterprise Houston Open yanaendelea kukua bila mipaka. 
 
"Wachezaji wetu walifurahi kuchezea katika bustani la Memorial Park lililoko katikati mwa Houston mwaka jana. Hii ni sehemu ambayo Jim Crane na wakfu wa gofu wa Astros wanajivunia sana”. 
 
Curtis Strange na Vijay Singh ndio wachezaji wenye mafanikio makubwa katika historia ya mashindano ya Houston Open  kwa kushinda mataji matatu. 
 

Washindi waliopita wa Houston Open.

 
2016 - Jim Herman –Marekani 
2017 - Russell Henley - Marekani
2018 - Ian Poulter -  Uingereza
2019 - Lanto Griffin - Marekani
2020 - Carlos Ortiz - Mexico 
 

Bashiri Gofu na Betway

Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 11/10/2021