Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 English Premier League
Matchday 14
Manchester United v Arsenal FC
Old Trafford Stadium
Manchester, England
Thursday, 2 December 2021
Kick-off is at 23h15
Uwanja wa Old Trafford utakuwa mwenyeji wa mtanange mkali wa mechi ya
ligi ya England Manchester United watakapowaalika Arsenal wikendi ya Disemba 2.
Hii itakuwa ni mara ya 59 baina ya timu hizo kukutana tangu kuasisiwa kwa ligi ya premier.
Manchester united wameonyesha ubabe wao kwa kushinda mara 24 dhidi ya 16 za Arsenal na kuambulia sare 18.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Timu hizi zilikutana mara ya mwisho katika mechi ya ligi Januari 30 na kuumiza nyasi pasipo sababu kwani mechi iliishia kwa sare ya 0-0.
Kwingineko, Manchester united walipoteza mechi yao ya mwisho wakiwa nyumbani kwa 2-0 dhidi ya mahasimu wao wa jadi Manchester City katika mechi iliyochezwa Novemba 6.
Kutokana na matokeo hayo, Manchester united iliendeleza msururu wa matokeo duni wakiwa nyumbani ikiwa wamerekodi sare moja na kushindwa mara tatu katika mechi nne za ligi.
Kwa upande mwingine, Arsenal walipoteza mechi yao ya mwisho ya ugenini dhidi ya Liverpool baada ya kichapo cha mabao 4-0 katika mechi iliyochezwa Novemba 20.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kichapo hicho kilivunja msururu wa timu ya Arsenal wa mechi tatu bila kushindwa ugenini huku wakiandikisha ushindi mara mbili na kupata sare moja.
"Anfield ni moja kati ya nyanja ngumu sana ulaya kwa wapinzani kupata matokeo mazuri. Ilikuwa sio wakati mwafaka kukutana nao katika hali waliyonayo sasa,” alisema meneja wa Arsenal Mikel Arteta baada ya kuchapwa na Liverpool.
"Walikuwa na kila sababu ya kushinda mechi hiyo. Sio njia nzuri ya kujifunza kwa kupoteza namna hiyo lakini tumejifunza mengi kutoka mechi hiyo kiukweli.
"Unapo poteza mechi namna hiyo, njia pekee ya kujifunza ni kuanza maandalizi ya mechi ifuatayo kwa wakati,” aliongeza.
"Tutachambua mechi hiyo kujua ni wapi tulikosea na kusabisha adhabu hiyo kisha tutarekebisha na kuelekeza nguvu kwenye mechi inayofuata.”
Takwimu baina ya timu hizi katika ligi, mechi tano zilizopita.
Mechi - 5
United - 0
Arsenal - 3
Sare - 2
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.