Man United inaonekana kuamka inapomualika mpinzani City.


Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 

2021/22 English Premier League

Matchday 11 of 38

Manchester United vs Manchester City 

Old Trafford 
Manchester, England
Saturday, 06 November 2021 
Kick-off is at 15:30 

Manchester United itafufua uhasama wake na mpinzani wake wa jadi Mnchester city katika mechi ya ligi ugani Old Trafford Jumamosi hii.

Pep Guardiola
Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 
 
Wikendi iliyopita, United waliibwaga Totenham Hotspus mabao 3-0 na kuvunja mkosi wa mechi nne za ligi bila ushindi na sasa wamechukua nafasi ya tano katika ligi. 
 
Matokeo hayo yamepunguza shinikizo kwa meneja wa United Ole Gunnar Solskjaer pamoja na mchezji Cristiano Ronaldo ambaye alifunga goli moja moja kwenye mechi hiyo.
 
"Timu ilikuwa na shinikizo kidogo kutokana na matokeo mabovu ya wikendi iliyopita. Tunajiamini na tulijua tutahitaji kushinda,” Ronaldo aliiambia Sky Sports

"Tulianza mechi vizuri. Najiskia faraja kwa sababu kazi yangu ni kusaidia wenzangu kwa kufunga magoli na kucheza vizuri na leo nimetimiza wajibu huo. Wachezaji wote walicheza vizuri kwa ujumla.”
 
Kwa upande mwingine, Manchester city ilipoteza mechi yao dhidi ya Crystal Palace kwa mabao 2-0 wakiwa nyumbani. Katika mechi hiyo, City walipoteza mchezaji mmoja kupitia kadi nyekundu na sasa wako nyuma ya viongozi Chelsea kwa alama tano baada ya mechi kumi.

"Utaelewa kwamba kucheza na wachezaji 11 dhidi ya 10 ni tofauti. Ni maamuzi aliyoona sahihi refa wa mchezo huo kutoa kadi nyekundu. Hata hivyo tulicheza vizuri kuliko mpinzani wetu licha ya kuwa na wachezaji kumi,” alisema mkufunzi wa Manchster city Pep Guardiola baada ya mechi hiyo.

"Ni vigumu sana kucheza na wachezaji kumi dhidi ya kumi na moja. Kipindi cha pili tulikuwa na dakika kama 25 za mchezo mzuri. Tulifunga goli na likakataliwa bila sababu,” aliongeza.. 
 
Bruno Fernandes
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Msimu uliopita, United walilazimisha sare ya 0-0 Old Trafford kabla ya kushinda mechi ya marudiano 2-0 katika uwanja wa City wa Etihad. Bruno Fernandes na Luku Shaw waikuwa wafungaji wa magoli ya united.
 

Takwimu baina ya Manchester United vs Manchester City katika ligi.

 
Mechi: 162
Manchester United: 65
Manchester City: 49
Sare: 48
 

Ratiba ya mechi za EPL mchezo wa siku ya 11

 
Ijumaa, 05 November
 
23:00 - Southampton vs Aston Villa 
 
Jumamosi, 06 Novembe
 
15:30 - Manchester United vs Manchester City 
18:00 - Chelsea vs Burnley 
18:00 - Crystal Palace vs Wolverhampton Wanderers 
18:00 - Brentford vs Norwich City 
20:30 - Brighton & Hove Albion vs Newcastle United 
 
Jumapili, 07 Novemba
 
17:00 - Everton vs Tottenham Hotspur 
17:00 - Leeds United vs Leicester City 
17:00 - Arsenal vs Watford 
19:30 - West Ham United vs Liverpool 
 
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
  
 

Published: 11/04/2021