Macho yote kuangazia 2021 RSM Classic


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021 RSM Classic 

US PGA Tour 

Sea Island Golf Club 
St. Simons, Georgia, USA
18-21 November 2021  
 
Mashindano ya gofu ya 2021 RSM Classic yatang’oa nanga Novemba 18 hadi 21, Sea Island Golf Club katika jimbo la Georgia nchini Marekani.
 
Haya yatakuwa Makala ya 12 ya mashindano ya golf ya PGA yaliyoasisiwa mwaka 2010. Makala hayo ya kwanza yalishindwa na Mmarekani Heath Slocum.
 
Kutokana na sababu za kiufadhili, mashindano haya yalibadilisha jina mwaka 2015 kutoka McGladrey Classic na kupewa jina la mfadhili mpya RSM US.

Jason Day
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Robert Streb ndiye bingwa mtetezi baada ya kushinda mashindano ya RSM Classic ya mwaka jana alipompiku Kevin Kisner katika raundi ya mchujo. 
 
Ushindi huo ulimfanya Robert Streb bingwa mara mbili wa PGA katika mashindano haya ya RSM Classic na ubingwa wa kwanza katika miaka sita. 
 
Streb atakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Jason Day, Jimmy Walker na Webb Simpson ambao wamethibitisha kushiriki mashindano ya mwaka huu. 
 
Kisner na Justin Rose ambao wote wamewai kuwa washindi wa mashindano haya watakuwa miongoni mwa washiriki. Mashindano haya yatachukua siku nne na yatajumuisha wachezaji 156. 

Justin Rose
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Wakfu wa Davis Love ndio muandaaji wa RSM Classic na wamechagua Peter Millar kuwa msambazaji wa pekee wa mavazi ya mashindano ya msimu wa 2021-2022.
 
“Tunayo furaha kuwa na Peter Millar kama mfadhili wa mavazi ya mashindano ya RSM Classic,” alisema Andy Bosman, meneja mkuu wa mauzo RSM. 
 
“Ushirikiano wetu na Peter Millar umekuwepo kwa zaidi ya miaka kumi. 
 
"Tumepokea maoni ya kutia moyo kutoka kwa usimamizi wetu, waajiriwa wetu na wateja wetu kuhusu huduma ya Peter Millar.”
 

Washindi watano wa mwisho wa mashindano ya RSM Classic

 
2016 - Mackenzie Hughes - Canada 
2017 - Austin Cook - Marekani
2018 - Charles Howell III - Marekani
2019 - Tyler Duncan - Marekani
2020 - Robert Streb - Marekani
 

Bashiri Gofu na Betway

Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 11/17/2021