Liverpool kuikabili timu ya Arsenal iliyoimarika zaidi


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2021/22 English Premier League

Matchday 12 of 38

Liverpool vs Arsenal 

Anfield 
Liverpool, England
Saturday, 20 November 2021 
Kick-off is at 20:30 
 
Liverpool watapania kuandikisha matokeo mazuri wakiwa nyumbani dhidi ya Arsenal katika mechi ya ligi jumamosi hii ugani Anfield. 

Mikel Arteta
Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 
 
Wekundu wa Anfield walipoteza mechi ya msimu kwa mara ya kwanza mikononi mwa West Ham united kabla ya ligi kuchukua mapumziko. Walipoteza mechi hiyo 3-2 na sasa wanajipata alama nne nyuma ya viongozi Chelsea na alama mbili mbele ya Arsenal wote wakiwa wamecheza mechi 11. 
 
"Haijalishi, lazima kuna kupoteza mechi. Maamuzi yetu kwa nyakati Fulani yalikuwa sio mazuri. Tunaweza kuimarika na nafasi tunayo ya kufanya hivyo,” alisema Jurgen Klopp wa Liverpool baada ya kupoteza mechi na West Ham. 
 
Kwa upande mwingine, Arsenal wamecheza mechi nane za ligi kwa mpigo bila kupoteza mechi yoyote. Wameshinda mechi tatu za mwisho huku ushindi wa karibuni ukiwa wa bao moja dhidi ya Watford. 
 
"Ni vizuri kupata ushindi kabla ya mapumziko ya ligi. Wachezaji wanaobaki klabuni wanakuwa na motisha,” alisema meneja wa Arsenal Mikel Arteta.  
 
"Ni lazima pia kutilia maanani wachezaji walioondoka kuziwakilisha nchi zao tunapojiandaa na  mikakati ya ligi itakaporudi.” 

Diogo Jota
Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 
 
Msimu uliopita, Liverpool walishinda mechi zote dhidi ya Arsenal na kutwaa alama zote sita katika mechi za ligi. Mechi ya kwanza walishinda 3-1 wakiwa nyumbani na kushinda 3-0 ugani Emirates. Diogo Jota alifunga katika mechi zote. 
 

Takwimu baina ya Liverpool na Arsenal

 
Mechi: 199
Liverpool: 75
Arsenal: 71
Sare: 53
 

Ratiba ya mechi za EPL, mchezo wa 12

 
Jumamosi, Novemba 20
 
15:30 - Leicester City vs Chelsea 
18:00 - Newcastle United vs Brentford 
18:00 - Burnley vs Crystal Palace 
18:00 - Aston Villa vs Brighton & Hove Albion 
18:00 - Watford vs Manchester United 
18:00 - Wolverhampton Wanderers vs West Ham United 
18:00 - Norwich City vs Southampton
20:30 - Liverpool vs Arsenal 
 
Jumapili, Novemba 21
 
17:00 - Manchester City vs Everton 
19:30 - Tottenham Hotspur vs Leeds United 

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 11/18/2021