Juventus na Atalanta kukabana koo


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Italian Serie A

Matchday 14

Juventus FC v Atalanta BC 

Allianz Stadium
Torino, Italy 
Saturday, 27 November 2021
Kick-off is at 20h00  
 
Juventus FC wataialika Atalanta BC ugani Allianz Stadium katika mchezo wa ligi kuu ya Italia Novemba 27.
 
Juventus, kwa jina la utani The Old Lady, walipata ushindi wa 2-0 wakiwa ugenini kwenye mechi iliyopita ya Novemba 20.
 
Kwa sasa, Juventus wameshinda mechi mbili zilizopita za ligi mfululizo.


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Katika mechi yao ya mwisho nyumbani, Juventus waliicharaza ACF Fiorentina baada ya US Sassuolo kuwapiga hapo awali ugani Allianz Stadium.
 
“Ni alama tatu muhimu ambazo tumepata. Tulitumia mbinu zilizotuwezesha kuwathibiti wapinzani pamoja na juhudi nyingi kutoka kwetu. Hayo yote yalitupa ushindi,” Massimiliano Allegri wa Juventus alisema baada ya ushindi huo dhidi ya Lazio.
 
“Mechi ya kwanza baada ya mapumziko ya ligi sio rahisi lakini tulijisatiti na kupata ushindi. Juventus ni timu kubwa, kwa hiyo ni lazima tuonyeshe mchezo wa kiwango chetu kama tulivyofanya leo.
 
"Tulianza msimu huu kwa matokeo mabaya lakini nina imani kwamba bado nafasi tunayo ya kufanya vyema zaidi. Nilifunga magoli leo lakini washambuliaji wetu walifanya kazi nzuri sana. “

Teun Koopmeiners
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kwa upande mwingine, Atalanta wakiwa nyumbani waliilemea Spezia kwa kuwachapa magoli matano kwa mawili. Mechi hiyo ya ligi ilichezwa Novemba 20.
 
Kwa mantiki hiyo, Atalanta hawajapoteza mechi yoyote kati ya sita za ligi zilizopita. Wameshinda mara nne mfululizo na kulazimisha sare mbili.
 
Vile vile, katika mechi kumi na mbili za ligi wakiwa nyumbani, Atalanta wameshinda mara tisa na kupata sare tatu.
 
Timu ya Juventus na Atalanta walikutana mara ya mwisho Aprili 18 2021.
 
Atalanta waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Juventus katika mechi iliyogaragazwa ugani Gewiss Stadium. 
 

Takwimu baina ya timu hizi katika mechi tano za mwisho za ligi.

 
Mechi - 5
Juventus - 1
Atalanta - 1
Sare - 3

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 11/23/2021