Juventus kutoana kijasho na Fiorentina


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Italian Serie A

Matchday 12

Juventus FC v ACF Fiorentina 

Allianz Stadium
Torino, Italy 
Saturday, 6 November 2021
Kick-off is at 20h00 
 
Juventus FC watakuwa wenyeji wa ACF Fiorentina katika mchezo wa ligi kuu ya Italia mnamo tarehe 6 Novemba ugani Allianz Stadium.
 
Katika matokeo ya kushangaza, Juventus walipoteza mechi yao ugenini dhidi ya Hellas Verona 2-1 mechi iliyochezwa oktoba 30. 
 
Katika mechi tatu za ligi zilizopita, Juventus wamepata sare moja na kupoteza mechi mbili mfululizo.

Massimiliano Allegri
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Sassuolo walivunja msururu wa ushindi wa mechi tatu kwa mpigo za Juventus wakiwa ugani Allianz Stadium.
 
“Kwenye mechi kama ya leo, ni sharti uwe na uwezo wa kucheza kiwango kimoja kama sio vizuri zaidi kuliko mpinzani wako,” alisema Massimiliano Allegri, meneja wa juventus baada ya mechi dhidi ya Verona. 
 
"Ushindi unapatikana unapocheza kwa kujituma zaidi kuliko mpinzani. Fikra zetu mwanzoni ni kwamba tulikuwa bora kuliko upinzani lakini matokeo yameonyesha tofauti. Verona walikuwa bora katika kila sekta kusema ukweli. Itabidi tupambane zaidi kuliko tulivyofanya leo.
 
"Huu ni muda wa kutazama hali yetu kwa jicho la tatu na kutafuta suluhu ya matokeo yetu. Wakati umefika juhudi zetu kuonekana kwenye matokeo.”

Jose Callejon
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kwengineko katika mechi ya ligi iliyochezwa Oktoba 31, Fiorentina ikiwa nyumbani iliitandika Spezia mabao 3-0.
 
Ushindi huu ulikuwa wa pili wa Fiorentina katika mechi tatu za ligi zilizopita baada ya kupoteza mechi yao dhidi ya SS Lazio.
 
Hata hivyo, rekodi ya Fiorentina wakiwa ugenini imekuwa ya kutamausha baada ya kupoteza mechi mbili za ligi kwa mpigo.
 
Mara ya mwisho timu hizi zilikutana Aprili 25 2021 katika mechi ya ligi.
 
Katika mchezo wa kusisimua, mechi hii iliishia sare ya 1-1 Fiorentina wakiwa nyumbani Stadio Artemio Franchi.
 

Takwimu baina ya timu hizi kwenye mechi tano za mwisho za ligi

 
Mechi - 5
Juventus - 2
Fiorentina - 1
Sare - 2

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 11/03/2021