Granada wapania kuwazima Madrid


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Spanish La Liga

Matchday 14

Granada CF v Real Madrid 

Estadio Nuevo Los Cármenes
Granada, Spain
Sunday, 21 November 2021
Kick-off is at 18h15
 
Granada CF itamenyana na Real Madrid katika mechi ya ligi kuu Uhispania Novemba 21 ugani Estadio Nuevo Los Cármenes. 
 
El Grana, kama wanavyojulikana Granada walipoteza mechi yao ya mwisho ya ligi ya tarehe 6 Novemba mikononi mwa Espanyol kwa magoli 2-1.  
 
Kabla ya mechi hiyo, Granada walikuwa na mechi nne mfululizo za ligi bila kupoteza huku wakiandikisha sare mbili na ushindi mara mbili. 

Robert Moreno
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Hata hivyo, katika mechi mbili za mwisho za ligi za nyumbani, Granada hawajapoteza mechi yoyote. Wameshinda mechi moja na kwenda sare mara moja.
 
Kwa upande mwingine, Madrid walishinda mechi yao dhidi ya Rayo Vallecano kwa magoli mawili kwa moja katika mchezo uliochezwa Novemba 6. 
Hivyo basi, Real Madrid hawajashindwa katika mechi ya ligi kati ya nne za mwisho walizocheza. Wameshinda mara tatu na kupata sare moja. 
 
Vile vile, Madrid wameshinda mechi mbili za mwisho za ligi walizocheza ugenini. 

Carlo Ancelotti
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Rayo hucheza vizuri sana lakini sisi hucheza vizuri zaidi kwa wapinzani wa sampuli hiyo. Tulicheza mchezo wa kushtukiza,” alisema mkufunzi wa Madrid Carlo Ancelotti baada ya ushindi huo dhidi ya Rayo. 
 
"Tulikuwa na mchezo mzuri katika mechi. Pengine ingekuwa  mechi ya msimu kama mechi ingemalizika mapema kidogo. 
 
"Tulitengeneza nafasi nyingi na tungefunga mabao zaidi. Hatukufanikiwa goli la tatu. Walifunga moja na kutupa tumbojoto kwa takriban dakika kumi hivi.” 
 
Mara ya mwisho katika ligi timu hizi kukutana ilikuwa Mei 13 2021. 
 
Madrid waliibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Granada katika mechi hiyo iliyochezewa Estadio Nuevo Los Cármenes. 
 

Takwimu baina ya timu hizi katika michezo mitano ya mwisho ya ligi

 
Mechi - 5
Granada - 0
Madrid  - 5
Sare - 0

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 
 

Published: 11/17/2021