Genoa kutonesha zaidi vidonda vya Milan


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Italian Serie A

Matchday 15

Genoa CF vs AC Milan

Stadio Comunale Luigi Ferraris 
Genova, Italy 
Thursday, 1 December 2021
Kick-off is at 21h45 CAT
 
Genoa CFC wataialika AC Milan katika mechi ya ligi kuu Italia ugani Stadio Comunale Luigi Ferraris Disemba mosi.
 
Hii itakuwa ni mara ya 32 baina ya timu hizi mbili kukutana katika mechi ya ligi tangu mwaka 1993.
 
Milan wameambulia ushindi katika mechi 18 dhidi ya 7 kwa faida ya Genoa huku nane kati ya mechi hizo zikiishia sare.

Brahim Diaz
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Vile vile, Rossoneri walishinda mechi ya mwisho ya ligi wakati timu hizo mbili zilikutana Aprili 18 2021.
 
Ushindi wa Milan dhidi ya Genoa ulikuwa wa 2-1 katika mechi hiyo ya ligi iliyochezewa kwenye uwanja wa Stadio Giuseppe Meazza.
 
Novemba 21, Genoa walipoteza mchezo wa ligi wakiwa nyumbani dhidi ya AS Roma kwa mabao mawili bila jawabu.
 
Matokeo hayo yanamaanisha Genoa wamepoteza mechi tano na kwenda sare mara tatu katika mechi nane za mwisho wakiwa nyumbani.

Cristian Zapata
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Hari ya wachezaji ilikuwa ya kutia moyo. Walicheza kama kikundi na kupigania timu kwa mapoja,” alisema Andriy Shevchenko meneja wa Geneo baada ya kipigo cha Roma.
 
"Hatukuweza kudhibiti mchezo vizuri, jambo ambalo tunahitaji kujifunza kufanya ili kutengeneza nafasi zaidi za kufunga mabao. Tunafahamu hilo lakini huu ndio mwanzo na nafasi ipo ya kutatua mapungufu haya.
 
"Ukizingatia uwezo wa wachezaji tulionao, safu ya ulinzi ya wachezaji watatu itatufaa zaidi lakini tutachambua kuona ni kipi kitafaa kulingana na hali. Nawashukuru pia mashabiki wetu kwa kuzidi kutushangilia na kutupa motisha.”
 
Katika mechi iliyochezwa Novemba 20, Milan walipoteza ugenini kwa mabao 4-3 dhidi ya ACF Fiorentina.
 
Ushinde huo ulifikisha kikomo msururu wa mechi tisa bila kushindwa kwa timu hiyo ya Milan ugenini huku wakiandikisha ushindi mara nane na kupata sare moja.
 

Takwimu baina ya timu hizi katika mechi tano za ligi za mwisho.

 
Mechi - 5
Genoa - 1
Milan - 3
Sare - 1


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 11/30/2021