Chelsea kuendeleza ubabe dhidi ya Man United.


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2021/22 English Premier League

Matchday 13 of 38

Chelsea vs Manchester United 

Stamford Bridge 
London, England
Sunday, 28 November 2021 
Kick-off is at 19:30  

Chelsea itapania kuzoa alama zote tatu itakapoialika Manchester United jumapili hii ugani Stamford Bridge katika mechi ya ligi.

Marcus Rashford
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Chelsea wanazidi kuongoza kwenye jedwali baada ya kuwapiga Leicester 3-0 wikendi iliopita na sasa hawajapoteza mechi yoyote ya ligi kati ya mechi sita zilizopita.

"Tumecheza mchezo mzuri na kupata matokeo mazuri tukiwa ugenini. Tulitengeneza nafasi nyingi,” alisema meneja wa Chelsea, Thomas Tuchel baada ya mechi hiyo.

"Tulifahamu vizuri uwezo wao na ilitubidi tujikaze vilivyo kuanzia mwanzo hadi mwisho na tulifanikiwa kufanya hivyo.”
 
United walimfuta kazi Ole Gunner Solskjaer baada ya timu hiyo kushindwa 4-1 na timu ya Watford. Kwa sasa, The Red Devils wamemteua Michael Carrick kukaimu nafasi hiyo huku wakiwa wamepoteza mechi tano kati ya saba za mwisho za ligi na sasa wameachwa kwa alama 12 na viongozi Chelsea.

"Ilikuwa huzuni kwangu na kwa wengine katika klabu yetu kushuhudia Ole akifukuzwa kazi,” alisema Carrick jumatatu alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari.

"Ulikuwa wakati mgumu kwangu kuandaa na kukutana na wachezaji kwa ajili ya mazoezi. Nafahamu muda ni mchache lakini hii ni changamoto nitakayoifanyia kazi.”

Christiano Ronaldo
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Msimu uliopita, timu hizi zilitoka sare ya 0-0 katika mechi zote mbili za ligi.
 

Takwimu baina ya Chelsea na Manchester United

 
Mechi: 171
Chelsea: 53
Manchester United: 69
Sare: 49
 

Ratiba ya mechi za premier league, mchezo wa 13.

 
Novemba 27, Jumamosi
 
15:30 - Arsenal vs Newcastle United 
18:00 - Liverpool vs Southampton 
18:00 - Norwich City vs Wolverhampton Wanderers 
18:00 - Crystal Palace vs Aston Villa 
20:30 - Brighton & Hove Albion vs Leeds United 
 
Novemba 28, Jumapili
 
17:00 - Brentford vs Everton
17:00 - Manchester City vs West Ham United 
17:00 - Leicester City vs Watford 
17:00 - Burnley vs Tottenham Hotspur 
19:30 - Chelsea vs Manchester United 

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 11/26/2021