Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 UEFA Champions League
Group F
Atalanta BC v Manchester United
Gewiss Stadium
Bergamo, Italy
Tuesday, 2 November 2021
Kick-Off 23h00
Baada ya kupata kichapo Old Trafford, Atalanta itakuwa na uchu wa kulipiza kisasi kwa Manchester United Novemba 2 katika
mchezo wa mabingwa wa kundi F.
Manchester united ilitoka nyuma na kushinda kwa mabao 3-2 dhidi ya Atalanta ugani Old Trafford kwenye mchezo uliopita wa kundi F Oktoba 20.
Matokeo hayo yalitia kikomo msururu wa matokeo mazuri ya Atalanta kwenye mashindano haya katika mechi mbili zilizopita ambapo wamepata sare moja na kushinda mechi moja.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Ushindi wa Atalanta dhidi ya Young Boys ya Uswizi ulikuwa wa kwanza katika mechi tano za ligi ya mabingwa walizocheza nyumbani.
“Tulishambulia kila tulipopata nafasi ya kufanya hivyo japo United walikaba sana,” alisema kocha wa Atalanta Gian Piero Gasperini baada ya kichapo cha Manchester United.
“Tuliwakosa baadhi ya wachezaji wetu jambo lililotukosesha uwezo wa kucheza kama tulivyoea. Hata hivyo, nawapongeza sana waliojaza nafasi hizo kwani walijituma kadri ya uwezo wao. United ni timu yenye uwezo mkubwa na tunajifunza mengi katika mechi kubwa. Sasa tunahitaji kujituma zaidi.”
“Timu sampli ya United inaweza kutengeneza nafasi katika hali yoyote na kusababishia upinzani matatatizo. Tungeongeza bao la tatu mapema pengine tungeshinda mchezo huo.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Wakati huo huo, Manchester United inapania kuendeleza msururu wa matokeo mazuri na kupata ushindi wa tatu katika mechi ya tatu mfululizo watakapokuwa ugenini dhidi ya Atalanta.
Manchester united wameandikisha ushindi katika mechi mbili zilizopita kwenye mashindano haya ya ligi ya mabingwa.
Hata hivyo, United hawajashinda mchezo wowote kati ya tatu za ligi hii ugenini huku wakipoteza mechi tatu zote.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Atalanta kuwaalika United katika mechi ya klabu bingwa barani Ulaya.
Takwimu baina ya timu hizi mbili katika ligi hii. (UEFA Champions League)
Mechi - 1
United - 1
Atalanta - 0
Sare - 0
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.